Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, ambae pia ni Mkuu Wilaya ya Songea, Pololet Mgema, akitoa hotuba katika Ufunguzi wa mafunzo na kuhamasisha zoezi la Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa Mifugo kwa Mikoa ya Tanzania bara katika Mkoa wa Ruvuma, kwa washiriki waliohudhuria mafunzo mafunzo hayo (hawapo pichani), kwenye ukumbi wa Songea Club, (kulia) Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Afya ya Jamii ya Mifugo, Dkt. Stanford Ndibalema, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Afya ya Jamii ya Mifugo, Dkt. Stanford Ndibalema, akitoa Elimu ya faida ya utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa Mifugo na kutoa ufafanuzi kuwa awamu ya pili ya utambuzi unafanyika kwa Teknolojia ya kisasa ambayo ni kuweka hereni ambazo itakuwa zikisajiliwa kwa njia ya mtandao, ametoa Elimu hiyo kwa wadau wa sekta ya Mifugo(hawapo pichani) kwenye ukumbi wa ofisi za Mkuu wa mkoa wa Ruvuma
Mkuu wa kitengo cha TEHAMA, Baltazar Kibora akitoa Elimu ya namna ya kutumia mfumo wa kielektronik (kwa kutumia kishkwambi) kutoa na kupata taarifa za utambuzi, Usajili na ufuatiliaji wa Mifugo kwa washiriki waliohudhuria kwenye mafunzo ya kuhamasisha zoezi la utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa Mifugo (hawapo pichani) katika Mkoa wa Ruvuma, mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Songea Club, Ofisi Mkuu wa mkoa
Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya kuhamasisha zoezi la utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa Mifugo katika mkoa wa Ruvuma, wakimsikiliza kwa makini mkufunzi wa mafunzo hayo, (hayupo pichani), katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa huo
...........................................................................
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanza mafunzo ya kuhamasisha zoezi la utambuzi, usajili na Ufuatiliaji wa Mifugo katika mikoa yote ya Tanzania, moja ya mikoa hiyo ambayo mafunzo hayo yanatolewa ni mkoa wa Ruvuma.
Akiongea katika Ufunguzi wa mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya songea, akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Pololet Mgema ametoa pongezi kwa Wizara kwa kuona umuhimu wa kutoa Elimu kabla ya zoezi hilo kufanyika, mafunzo hayo yamefanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma .
Mgema amesema Mfumo wa utambuzi na Ufuatiliaji Mifugo Tanzania unasimamiwa kwa Sheria ya Usajili, utambuzi na Ufuatiliaji Mifugo Na. 12 ya mwaka 2020 na kanuni zake za mwaka 2011, na kwa Mkoa wa Ruvuma, Halmashauri ziko kwenye hatua tofauti ya maandalizi ya kutekeleza zoezi hilo.
"Nitoe rai kwa wafugaji wote walioko katika Mkoa wa Ruvuma kutoa Ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha zoezi la utambuzi kwa njia ya hereni kwa Mifugo yenu", amesema Mgema.
Ameongezea kwa kusema ni muhimu wafugaji Waelewe zoezi hilo na kuchangia utekelezaji wake, na hakuna uchaguzi kama tunataka kuelendelea kuwa wafugaji wa zama hizi za sasa na zijazo.
Aidha, ameomba Wizara kushirikiana na wadau mbalimbali wa Maendeleo, Viongozi wa Halmashauri, chama cha wafugaji na wataalam wa Mifugo ili kutatua changamoto ya migogoro baina ya wakulima na wafugaji, kwani wafugaji wengi hawana maeneo ya kuchungia.
Naye Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Afya ya jamii ya Mifugo, Dkt. Stanford Ndibalema amesema mwaka 2017, wizara ilianza na kutambua Mifugo kwa kutumia alama za chapa ya moto, ambazo kila kila Kijiji kilikua na namba, lakini zoezi hilo liligubikwa na changamoto ya alama kufutika na malalamiko ya kuharibu Ngozi, na ya kukiuka ustawi wa wanyama kwakuwa ule moto unaumiza wanyama.
Ndibalema ameongezea kwa kusema kwa kuona hivyo serikali ikaja na utaratibu mzuri wa kutumia mfumo kielektronik unaofuatwa kwa kuvalisha Mifugo hereni kwenye sikio.
Naye Afisa Mifugo kutoka Halmashauri ya Mbinga, Haruna Masige ametoa wito kwa wafugaji wawe kupokea zoezi hilo la utambuzi kwakuwa lina faida kubwa ikiwapo kuzuia wizi na inatoka Fursa kwa serikali kupanga Mipango thabiti kwa nchi nzima,
Pia, Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri ya Mbinga, Grace Quitine amekiri kupokea mafunzo hayo na anaimani mafunzo hayo ya tawezesha viongozi kwenda kutoa Elimu kwa wafugaji ili naweza kusajili Mifugo yao na ili kuleta faida ya kuweza kupata Masoko hata nje ya nchi na kuweza kuongeza pato la nchi kwa ujumla.
Social Plugin