Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Lazaro Nyanga magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema amekabidhi magodoro ili kukabiliana na uhaba wa malazi unaotokana na changamoto ya msongamano wa wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga.
Mhe. Mjema amekabidhi magodoro 50 kati ya 100 yaliyotolewa na Kampuni ya GSM leo Jumatano Desemba 22,2021 kwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Lazaro Nyanga ikiwa ni sehemu ya jitihada anazofanya katika kuondoa changamoto zilizopo kwenye magereza.
“Wafungwa wanakwenda gerezani kwa ajili ya kujifunza kutokana na makosa waliyofanya. Ni sawa wametenda makosa lakini kuwa gerezani haimaanishi kwamba wakose haki zao ndiyo maana serikali inaendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuondoa changamoto zilizopo magerezani na kutokana na hali hiyo nimefanikiwa kupata magodoro 100 kutoka Kampuni ya GSM, na leo nakabidhi magodoro 50 na mengine yatakuja ili yakatumike kuondoa changamoto ya malazi gerezani”,amesema Mjema.
“Msongamano katika gereza la wilaya ya Shinyanga ni mkubwa ambapo mahabusu na wafungwa wanafika takribani 450 na mkoa mzima idadi ni zaidi ya 800 hivyo ni lazima tufanye jitihada za kuhakikisha wanapata malazi. Naomba wadau wengine wajitokeze kutoa mahitaji mbalimbali kwenye magereza yetu ili waishi vizuri”,ameongeza Mjema.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema kwa jitihada anazoendelea kuzifanya kuondoa changamoto katika maeneo mbalimbali ikiwemo kutatua changamoto ya msongamano magerezani.
“Hivi sasa tunaendelea na jitihada za kujenga bweni ‘sero’ mpya ya magereza yenye uwezo wa kubeba mahabusu/wafungwa 100. Naomba wadau wajitokeze kuchangia ujenzi huu pamoja na kuendelea kusaidia mahitaji mbalimbali katika magereza. Tumekuwa tukiona hata nyakati za Sikukuu wadau wamekuwa wakifika kwenye magereza na kutoa misaada na zawadi tunawashukuru sana, naomba tuendelee na moyo huo”,amesema Mboneko.
Akipokea Magodoro hayo, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Lazaro Nyanga amemshukuru Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema kwa kufanikisha kupatikana kwa magodoro ambayo yatasaidia kupunguza changamoto ya malazi katika Gereza la wilaya ya Shinyanga ambalo lina msongamano mkubwa wa mahabusu na wafungwa.
Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Shinyanga, William Makwaya amesema gereza hilo lina uwezo wa kubeba wafungwa na mahabusu wa kiume 130 na wa kike 30 (jumla 160) lakini idadi imekuwa ikipanda hadi kufikia zaidi ya 450 ambapo leo Desemba 22,2021 wapo 439 huku akibainisha kuwa changamoto iliyopo kuwa ni malazi kwani magodoro ni machache.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Lazaro Nyanga magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga leo Jumatano Desemba 22,2021 katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Lazaro Nyanga magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kushoto) akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Lazaro Nyanga magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akikabidhi magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akikabidhi magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Lazaro Nyanga (kushoto) akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akikabidhi magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga
Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Shinyanga, William Makwaya akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akikabidhi magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akikabidhi magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akikabidhi magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga
Awali Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Lazaro Nyanga (katikati) akiangalia sehemu ya magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Lazaro Nyanga (kushoto) na Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Shinyanga, William Makwaya wakikagua magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akisalimiana na maafisa wa Jeshi la Magereza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akisalimiana na maafisa wa Jeshi la Magereza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin