Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RUFAA YA OLE SABAYA KUANZA KUSIKILIZWA FEBRUARI MWAKANI


Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha imepanga kuanza kusikiliza rufaa iliyofunguliwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili Februari 14, 2022.

Sabaya kupitia mawakili wake wamekata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa Oktoba 15 mwaka huu na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha, Ruth Massam amesema leo Desemba 13, 2021 rufaa hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na kupangiwa tarehe ya kuanza kusikiliza.

Amesema rufaa hiyo itakayosikilizwa mfulululizo itaanza Februari 14 mwakani mbele ya Jaji atakayekuwa amepangiwa.

"Leo imekuja kwa ajili ya kupanga tarehe ya kuanza kusikilizwa. Itaanza kusikilizwa Februari 14, 2022 mbele ya Jaji atakayepangiwa na itaendelea mfulululizo kama mtakavyoelekezwa,"amesema

Rufaa hiyo namba 129 ya mwaka huu, wajibu Rufaa (Jamhuri), waliwakilishwa na jopo la mawakili wanne wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Tumaini Kweka, Mawakili wa Serikali Waandamizi Ofmed Mtenga, Felix Kwetukia na Wakil wa Serikali Baraka Mgaya.

Waomba rufaa ambao ni Sabaya, Sylvester Nyegu na Daniel Mbura, waliwakilishwa na Mawakili Mosses Mahuna, Sylvester Kahunduka na Fauzia Mustapha.

Wakili Mahuna aliieleza mahakama kuwa rufaa hiyo imekuja kwa ajili ya kutaja na wako tayari kupokea amri zingine za mahakama..


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com