SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI YA WANAKWAYA 33 WALIOFARIKI MTONI


Gavana wa kaunti ya Kitui nchini Kenya  Charity Ngilu amesema kuwa serikali ya kitaifa na ile ya kaunti yake zitagharamia mazishi ya waathiriwa wa mkasa wa basi uliotokea katika daraja la Mto Enziu kaunti Jumamosi.

Akizungumza Jumanne ya Disemba 7,2021 Ngilu alisema kuwa Wizara ya Mambo ya Ndnai kupitia kwa Mamlaka ya Kudhibiti Majanga ya Kitaifa ilikuwa inashughulikia jinsi ya kuwasitiri jamaa za walioangamia.

 “Serikali ya kitaifa inashughulika kuhakikisha kuwa familia za waliohusika katika ajali hiyo zinasaidiwa. Kama kaunti, pia tutasaidia familia zilizopoteza wapendwa wao,” Ngilu alisema.

 Ngilu aliutenga uongozi wake na ukarabati wa daraja hilo la maafa, akisema lilikarabatiwa na Mamlaka ya Barabara Mashinani (KURA).

Kwa mujibu wa Ngilu, serikali ya kaunti hushughuilikia barabara zinazounganisha vijiji na wala sio barabara kubwa kama ile. “Kandarasi ya kazi hii ilikuwa ishatolewa, ni miaka sasa. Mkandarasi alifanya kazi chwara na kuondoka. Hii ni kazi ya KURA,” Ngilu alisema.

Ngilu vilevile alidokeza kuwa serikali itashughulikia ukabarati wa daraja hilo akiongeza tayari mipango ya kufufua daraja hilo ilikuwa imeanza.

 “Naamini kuwa serikali itachukua hatua madhubuti ili kuhakikisha kuwa daraja hili haliwi tena kitovu cha maafa. Najua litafanyika. Serikali ya kitaifa tayari imelizamia,” alisema. 

Watu 33 wakiwemo watoto wanne walipoteza maisha yao baada ya basi walilokuwa wameabiri kuelekea katika hafla ya harusi kutumbukia mto Enziu. Dereva alikuwa anajaribu kuvuka daraja hilo liliokuwa limefurika lakini akazidiwa na maji na basi hilo kubingiria mtoni pamoja na abiria.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post