************************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Simba Sc imefanikiwa kufuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho mara baada ya kufanikiwa kushinda kwa jumla ya mabao 4-2 dhidi ya timu ya Red Arrows Fc katika mechi zote mbili licha ya mchezo wa leo kuchapwa mabao mawili kwa sufuri.
Mechi ya kwanza Simba akiwa nyumbani aliweza kupata mabao 3-0 kwenye mchezo ambao ulikuwa wa aina yake, hivyo kutokana na leo kuchapwa mabao 2-1 wanakuwa na jumla ya mabao 4-2 hivyo wanakwenda hatua ya makundi moja kwa moja.
Red Arrows Fc katika mchezo huu walicheza kandanda safi lililovutia lakini haikuwafanya kuwazuia Simba Sc kufuzu hatua ya makundi.
Social Plugin