Baada ya kuondoka kwa Da Rosa, Hitimana aliendelea na kibarua chake kama msaidizi wa Pablo Franco aliyefanikiwa kuifikisha Simba kwenye hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho.
Wekundu wa Msimbazi, ilifikia makubaliano ya kuvunja kandarasi baina ya pande mbili na mkufunzi huyo raia wa Rwanda kwenye ofisi za klabu zilizopo Masaki, Dar es salaam.
Hitimana mwenye uzoefu wa soka la Tanzania amewahi kufundisha, Namungo FC aliyoachana nayo mwaka 2020 mwezi novemba, pia amewahi kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Rwanda ya U-23 mwaka wa 2012 na baadaye Rayon Sports kabla ya kuinoa Bugesera FC kama kocha mkuu mwaka wa 2018.
Pia Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mulamu Ng'ambi amekanusha taarifa zinazoenea kuwa mabingwa hao wapo mbioni kuachana kiungo wao Mkabaji, Raia wa Uganda, Taddeo Lwanga aliyekuwa akikabiliwa na majeraha, kuwa bado yupo sana Injia huyo atajiunga na wenzake kwenye uwanja wa mazoezi baada ya kupona.
Chanzo - EATV
Social Plugin