Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA KRISMASI KWA MAJIRANI ZAKE CHAMWINO

Kaimu Mkurugenzi huduma za Ikulu Daniel Mwalusamba akitoa zawadi kwa niaba ya Rais Samia kwa watu wasioona Buigiri
**
Na Dotto Kwilasa Malunde 1 blog, DODOMA.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi mbalimbali kwa wakazi wa kituo cha wasioona Watu wazima Buigiri-Matembe Bora ,kilichopo kata ya Buigiri,Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Akizungumza kwa niaba ya Rais mara baada ya kukabidhi zawadi hizo leo,Kaimu Mkurugenzi Huduma za Ikulu Daniel Mwalusamba amesema lengo la zawadi hizo ni kushiriki pamoja na makundi maalumu katika kusherehekea sikukuu ya Chrismasi na Mwaka mpya.

"Zawadi hii ni sehemu ya salamu za Krismasi ambayo imetolewa na Mama yetu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kuwajali jirani zake na watu wenye mahitaji maalumu",amesema.

Mwalusamba pia amesema,Rais Samia anawatakia heri ya sikukuu njema watu hao na kwamba wanapaswa kusherehekea kwa amani na utulivu.

Sambamba na hayo ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa Wadau mbalimbali wa maendeleo nchini kuendelea kusaidia watu wenye mahitaji maalumu katika kipindi hiki cha Sikukuu ikiwa ni ishara ya kuwaenzi hali itakayowatoa kwenye upweke.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kituo hicho Yared Cheleso amemshukuru Rais Samia kwa zawadi hizo na kueleza kuwa huo ni upendo unaopaswa kuigwa na wadau wengine huku akimtakia heri ya afya njema na utendaji mwema wa kazi.


Mbali na hayo wamemtoa hofu Rais kwamba wao kama watu wenye ulemavu wa macho wamekuwa na matumaini na uongozi wake na wapo pamoja katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona kwa kila hatua.

"Wewe ni mama yetu,tunakuamini endelea kufanya kazi na sisi tupo nyuma yako,katika mapambano haya ya Uviko 19 tupo pamoja na tunajitahidi kufuata hatua zote za kujikinga na kuwaelimisha wengine,"amesema.

Kaimu Mkurugenzi huduma za Ikulu Daniel Mwalusamba akitoa zawadi kwa niaba ya Rais Samia kwa watu wasioona Buigiri

Kaimu Mkurugenzi huduma za Ikulu Daniel Mwalusamba akitoa zawadi kwa niaba ya Rais Samia kwa watu wasioona Buigiri

Kaimu Mkurugenzi huduma za Ikulu Daniel Mwalusamba akizungumza baada ya kutoa zawadi kwa niaba ya Rais Samia kwa watu wasioona Buigiri

Mwenyekiti wa Kituo hicho Yared Cheleso akimshukuru Rais Samia kwa zawadi za Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2022

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com