Tamasha la muziki la nyota wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Koffi Olomide, lililotarajiwa kufanyika Desemba 11, jijini Nairobi limekatishwa.
Wanaharakati waliomba onyesho hilo lisiendelee kutokana na sifa yake ya kuwanyanyasa wanawake.
Waandalizi wa tamasha la Kenya wameahidi kurejesha pesa kamili kwa mashabiki waliokuwa tayari wamenunua tiketi za onyesho hilo, wakitaja sababu kadhaa za kuhairishwa kwa tamasha hilo.
Mnamo mwaka wa 2019, mwimbaji huyo wa Soukus wa DRC ambaye jina lake halisi ni Antoine Agbepa Mumba alipatikana na hatia ya ubakaji wa mmoja wa wachezaji densi wake wa zamani wakati binti huyo akiwa na umri wa miaka 15.
Amekuwa matatani na sheria mara kadhaa hapo awali kwa kumvamia mmoja wa wachezaji wake katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.
Social Plugin