Hizi ni ripoti kutokea Maharashtra, nchini India, ambapo kundi la tumbili limelipiza kisasi kwa kuwaua mbwa wapatao 250, baada ya kukasirishwa na kitendo cha mbwa kumuua kichanga chao.
Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa, tumbili hao walitekeleza mauaji hayo kwa kuwakamata mbwa na kupandanao juu ya miti kwenye nyumba na kisha kuwatupa chini.
Tayari mamlaka za wanyama pori nchini humo zimefika eneo la tukio na kuwakamata tumbili hao na kuwaweka kwenye uangalizi maalumu.
Ushawahi kukutana na timbwili la tumbili?
Social Plugin