Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

VILIO NA SIMANZI VYATAWALA MWILI WA MWANAFUNZI WA SUA ALIYEUAWA UKIAGWA MOROGORO


Vilio na Simanzi vimetawala wakati wa ibada ya kumuaga Mwanafunzi ambaye amehitimu katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro, Magreth Mashuwe aliyeuawa na watu wasiojulikana katika mashamba ya chuo hicho hivi karibuni huku chanzo kikikwa bado hakifahamiki.

Ibada hiyo imefanyika katika viwanja wa Mochwari ya Hospitali ya Rufaa mkoa Morogoro ambayo imehudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki.

Akizungumza mara baada ya ibada hiyo, Dada wa marehemu Liliani Mashuwe amesema mazishi yanatarajia kufanyika katika Kijiji cha Shimbikati kata ya Mkuu, wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro Disemba 23, 2021. Anasema wao kama familia wanaziachia mamlaka husika kufuatilia tukio hilo ili kuwabaini waliohusika.

Kwa upande wake Mchungaji wa kanisa la Tanzania Assemble of God (TAG) Dismas Kimario amewataka ndugu wa marehemu kumshukuru Mungu kila jambo kama maandiko ya Biblia takatifu yanavyosema.


Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) mkoa wa Morogoro, Ralph Meela alisema kuwa Msichana huyo alikua anasona Chuo kikuu Cha SUA Kozi ya Sayansi ya Mazingira na kufanikiwa kufanya mahafali Novemba 26, 2021 na Disemba 14 alipotea hadi Disemba 18 mwili wake ulipopatikana katika mashamba ya Chuo hicho.


Meela alisema uchunguzi wa awali unaonesha shingo ya marehemu imelegea huenda ikiwa ndo chanzo cha kifo chake huku upelelezi ukiendelea kuwabaini waliohusika na kifo chake na kwamba hadi sasa wanamshikilia mtu mmoja katika tukio hilo ambaye alikua rafiki yake wa kiume.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com