Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt.Francis Michael
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU nchini Neema Mwakalyelye
**
Na Dotto Kwilasa,Malunde 1 Blog-DODOMA.
WADAU wa mapambano dhidi ya rushwa nchini wametoa mapendekezo kwa Serikali kuona haja ya kuangalia upya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa zilizopo sasa hali itakayosaidia kuwabana zaidi viongozi wasio waadilifu.
Haya yamejiri jijini Dodoma wakati wa kikao cha Wadau wa mradi wa mapambano dhidi ya rushwa ujulikanao “Tuungane kutetea haki awamu ya pili unaotekelezwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini(TAKUKURU)kwa kushirikiana na shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS)kutoka nchini Ujerumani.
Wakizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kikao hicho,mwenyekiti wa kikao hicho Dkt. Francis Michael ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora amesema kutaifisha pekee kwa mali za viongozi wala rushwa haitoshi hivyo kuna haja kubwa ya kuangalia upya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU nchini Neema Mwakalyelye ameeleza lengo la mradi huo kuwa ni kuwashirikisha wadau ngazi za vijiji na mitaa hadi taifa namna ya mapambano dhidi ya rushwa .
Amesema ikiwa Viongozi wa ngazi za chini wataelimishwa na kuelewa madhara ya rushwa itasaidia kwa wananchi wengine kuelimika na kuacha vitendo vya rushwa.
Meneja mradi wa KAS Tanzania Damas Nderumaki naye ameeleza matarajio ya mradi huo kwa sasa ni kufikia mikoa 24 .
"Tayari tumefikia mikoa tisa na mafanikio yanaonekana,wa manchi wanaanza kuelimika na kujifunza zaidi faida za kukà taa kutoa rushwa,tunawaekimisha kuwa wanatakiwa kujielewa na kutambua kuwa umuhimu wa kupewa haki ya huduma za jamii ni bure na hauhitaji rushwa,"ameeleza
Kwa upande wao baadhi ya wadau wa mradi wa Tuungane wameeleza kuwepo kwa mazingira magumu ya kuwabaini na kuwafichua Wala rushwa hivyo kuomba kuwepo kwa marekebisho zaidi ya kisheria ili kuruhusu urahisi wa kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.
Naibu Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania Abdallah Sakasa,amesema mara nyingi Viongozi watuhumiwa wa rushwa wanapo bainika hutakiwa kutaifishwa mali zao na kuendelea kubaki kwenye nafasi zao jambo ambalo amesema linatia shaka .
"Tunataka marekebisho zaidi ya sheria ,mtu akibainika anatakiwa kujiuzulu nafasi yake na kutaifishwa mali zote Kisha afikishwe kwenye sheria ili iwe fundisho kwa wengine,watu hawa tusiwaangalie kwa macho ya huruma kwani ni sawa na wauaji,"amesema.
Naye Mbunge wa Mbagala jijini Dar es Salaam Abdallah Chaurembo amesema kuwa kikao hicho kimekuwa na mchango mkubwa na kinatarajiwa zaidi kuchochea mapambano dhidi ya rushwa kwani kimetoa nafasi kwa wadau kujadili namna ya kudhibiti uhalifu wa Kutoa na kupokea rushwa.
"Tumejifunza na kujadili mambo mengi,kila mtu anatakiwa kutimiza wajibu wake kama mwana jamii ili kuweka usawa,hakuna asiyejua kuwa rushwa ni adui wa haki hivyo ili haki ioatikane katika huduma zote za kijamii ni lazima kila mmoja akubali kuzuia rushwa na kuikataa kwa vitendo,"amesisitiza.
Kwa upande wake Afisa Uchunguzi - TAKUKURU Wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora Ilandike Julius ameeleza kuwa kikao hicho kimeleta matumaini Kwa jamii huku akiwataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa weledi, uaminifu na uadilifu ili waweze kuleta matokeo chanya katika sekta mbalimbali za kimaendeleo bila kula rushwa.
Pia amewataka wafanyakazi kutoa huduma kwa wananchi kwa kufuata taratibu zilizowekwa pamoja na kusimamia vizuri fedha za miradi ya maendeleo zinazopelekwa katika maeneo yao.
"Rushwa ni adui wa haki, utu na heshima ya binadamu,watumishi hakikisheni mnaridhika na mishahara yenu naamini wa kufanya hivyo hakuna atakaye penda rushwa,lakini pia mnao shawishi rushwa epukeni hiyo ni dhambi kama dhambi nyingine,"amesisitiza.
Social Plugin