Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WADAU WAJADILI MIKAKATI YA KAMPENI SHIRIKISHI YA KINGA DHIDI YA UVIKO 19…HALMASHAURI KUCHANJA WATU 500 KILA SIKU SHINYANGA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza wakati akifungua kikao cha wadau kwa ajili ya kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mkoa wa Shinyanga unatarajia kuchanja watu wapatao 1,196,153 (60%) ifikapo mwezi Juni, 2022 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Shirikishi na Harakishi wa utoaji wa chanjo awamu ya pili ambapo kila halmashauri inatakiwa ichanje watu kuanzia 500 na kuendelea kwa siku ili kuweza kufikia lengo hilo.

Hayo yamesemwa leo Desemba 31,2021 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary wakati akifungua kikao cha wadau juu ya Utekelezaji wa mpango shirikishi na harakishi kuhusu utoaji wa chanjo dhidi ya uviko-19 awamu ya pili mkoa wa Shinyanga kilichoandaliwa na Shirika la Tanzanian Men as Equal Partner in Development (TMEPiD) kwa ufadhili wa UNFPA.

Omary ameeleza kuwa moja ya mikakati ya kufanikisha mpango huo ni kushirikisha wadau wote pamoja rasilimali zilizopo kuhakikisha jamii inapata uelewa na kuongeza uhitaji wa chanjo hivyo amewaomba wadau waongeze nguvu katika maeneo ya uhamasishaji kwa kuishirikisha jamii ili kufikia lengo katika Mkoa wa Shinyanga.

Katibu Tawala huyo wa mkoa amesema kwa kuzingatia ufanisi mkubwa wa utekelezaji wa Mpango Shirikishi na Harakishi wa utoaji wa chanjo awamu ya kwanza, Serikali imeweka Mpango Shirikishi awamu ya pili wenye lengo la kuchanja asilimia 60 ya watu wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea ifikapo Juni, 2022.

“Katika utekelezaji wa Mpango Shirikishi na Harakishi wa utoaji wa chanjo awamu ya pili Mkoa wa Shinyanga unatakiwa kuchanja watu wapatao 1,196,153 (60%) ifikapo Juni, 2022. Tumelekezwa kila halmashauri ichanje watu kuanzia 500 na kuendelea kwa siku ili kuweza kufikia lengo hilo”,amesema Omary.

“Kupitia kikao hiki, naelekeza chanjo iwe kipaumbele kwa kila mmoja wetu hivyo Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi mshiriki na kusimamia zoezi hili na kuhakikisha kila mwananchi mwenye umri kuanzia miaka 18 anahamasika na kupatiwa chanjo ,wanasiasa wote katika ngazi tofauti mnaombwa kushirikiana na watoa huduma za Afya kufanya uhamasishaji na kuwashawishi wananchi kupata chanjo”,amesema.

"Ninaishukuru serikali kwa kuhakikisha chanjo hizi zinakuwepo muda wote ili wananchi wapate chanjo.  Serikali inatumia rasilimali nyingi katika masuala ya chanjo ya Uviko – 19 hivyo hatutamvumilia mtu yeyote atakayehamasisha watu wasichanje.Tutawachukulia hatua kali wale watakaokwamisha zoezi la utoaji chanjo”,amesema Omary.

“Naelekeza pia mtu yeyote atakayepotosha kuhusu chanjo ya UVIKO-19 ndani ya Wilaya za Mkoa wa Shinyanga Wakuu wa Wilaya shughulikie suala hilo na kila mwananchi kuwa sehemu ya uhamasishaji wa chanjo dhidi ya Uviko – 19”,ameongeza.

Amesisitiza kuwa tatizo la ugonjwa wa UVIKO – 19 bado lipo, na serikali inaendelea kuhakikisha wananchi wake wanapata kinga kupitia chanjo, hivyo inaendelea kuhakikisha chanjo zinapatikana na kutolewa.

Ameongeza kuwa Mkoa wa Shinyanga umeendelea kupokea chanjo kwa ajili ya kujikinga na UVIKO – 19 kwa awamu tofauti tofauti na kwamba hadi kufikia tarehe 25/12/2021 Mkoa umepokea jumla ya Dozi 88491 baada ya kumaliza dozi za awamu ya kwanza.

Hata hivyo amesema katika awamu iliyopita miongoni mwa changamoto walizozibaini ni kuwepo kwa uelewa mdogo wa jamii juu umuhimu wa chanjo ya UVIKO – 19, imani potofu na uvumi usio sahihi juu ya chanjo miongoni mwa jamii na baadhi ya viongozi wa dini, siasa na serikali kutotoa ushirikiano na kupotosha jamii kuhusu chanjo ya Uviko 19.

“Kutokana na muitikio mdogo wa jamii, serikali ilikuja na mpango mkakati unaoitwa Mpango Shirikishi na Harakishi wa utoaji wa chanjo ya UVIKO-19 kwa jamii “Accelerated Community Based Covid-19 Vaccination Strategy” kwa lengo la kufikia kiwango cha asilimia 100 cha utoaji wa chanjo zote zilizopokelewa ndani ya siku 20 kuanzia tarehe 01/10/2021 hadi tarehe 20/10/2021”,amefafanua.

“Kupitia mpango huo ambao ulioanza kutekelezwa rasmi tarehe 27/09/2021 Mkoa wa Shinyanga uliongeza vituo vya kutoa huduma ya chanjo hiyo kutoka vituo 18 hadi vituo 208 na ukaweka mkakati wa kumaliza chanjo tarehe 10/10/2021 ambapo ulifanikiwa kumaliza tarehe 14/10/2021.

Nipende kuwashukuru wote kwa umoja wetu kuweza kufanikisha kumaliza chanjo zote ndani ya muda uliokuwa umepangwa na Serikali, kwa pamoja tunaweza, na sasa tumeanza kutekeleza awamu ya pili”,amesema

“Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau inaendelea na utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kupambana na ugonjwa wa UVIKO – 19. Serikali iliongeza mkakati wa kutoa chanjo kwa wananchi ikiwa ni moja ya njia ya kupambana na ugonjwa huo. Naomba wananchi mjitokeze kupata chanjo kwani Kinga ni bora kuliko tiba, chanjo dhidi ya Uviko-19 ina ubora, usalama na ufanisi wa kutosha”,amesema Omary.

Mratibu Miradi wa Shirika la TMEPiD, John Maliyapamba Komba amesema wao ni wadau wa maendeleo hivyo wataendelea kushirikiana na serikali pamoja wadau mbalimbali ili kuwa na jamii yenye afya na iliyo huru dhidi ya maambukizi ya UVIKO 19.

Naye Mratibu wa Chanjo ya UVIKO 19 Mkoa wa Shinyanga Timoth Sosoma amesema lengo la mpango shirikishi na harakishi awamu ya kwanza ilikuwa ni kuongeza uelewa,kuikubali na kuongeza matumizi ya chanjo na kufikia asilimia 100 ya chanjo zilizokuwepo na sasa awamu ya pili ni kufikia asilimia 60 ya wananchi katika mkoa.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Daniel Mzee amesema lengo la kikao hicho ni kufanya uhamasishaji kuhusu utoaji chanjo,kukumbushana wajibu wa kukabiliana na UVIKO – 19 na chanjo ya UVIKO 19 wa wajumbe kufahamu mpango mkakati wa shirikishi na harakishi wa utoaji wa chanjo kwa jamii awamu ya pili.

Nao washiriki wa kikao wameshauri Wenyeviti wa serikali za mitaa na maafisa maendeleo ya jamii, viongozi wa dini,mila,siasa na waandishi wa habari wasiachwe nyuma katika uhamasishaji  elimu ya utoaji  chanjo ya Uviko 19 na kupuuza upotoshaji wa radio za mbao na mitandao ya kijamii kuhusu chanjo.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza wakati akifungua kikao cha wadau kwa ajili ya kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza wakati akifungua kikao cha wadau kwa ajili ya kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza wakati akifungua kikao cha wadau kwa ajili ya kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi akizungumza katika kikao cha wadau kwa ajili ya kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.
Kaimu Mganga Mkuu wa Shinyanga Dkt. Daniel Mzee akizungumza katika kikao cha wadau kwa ajili ya kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.

Mratibu Miradi wa Shirika la TMEPiD, John Maliyapamba Komba akizungumza katika kikao cha wadau kwa ajili ya kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.

Mratibu wa Chanjo ya UVIKO 19 Mkoa wa Shinyanga Timoth Sosoma akizungumza katika kikao cha wadau kwa ajili ya kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.

Wadau wakiwa kwenye kikao cha kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.

Wadau wakiwa kwenye kikao cha kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com