Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAFUGAJI KATAVI WAKUBALI UTAMBUZI WA MIFUGO KWA KUTUMIA HERENI ZA KIELEKTRONIKI


Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Udhibiti wa Magonjwa yaenezwayo na Wadudu kutoka WMUV, Dkt. Benezeth Lutege akiwaeleza wafugaji kuhusu umuhimu wa kuvalisha hereni mifugo katika mnada wa Itenge uliopo kwenye Kijiji cha Itenga A, Kata ya Itenga, Wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi.


Clarence Francis kutoka Kitengo cha Uhasibu (WMUV) akimuelezea mmoja wa wafugaji waliofika kwenye mnada wa Itenge uliopo kwenye Kijiji cha Itenga A, Kata ya Itenga, Wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi juu ya umuhimu wa uvalishaji hereni kwenye mifugo.


Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Udhibiti wa Magonjwa yaenezwayo na Wadudu kutoka WMUV, Dkt. Benezeth Lutege akimvalisha hereni ng’ombe kwenye mnada wa Itenge uliopo kwenye Kijiji cha Itenga A, Kata ya Itenga, Wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi.


Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Katavi, Nehemia James akijibu swali lililoulizwa na mmoja wa wafugaji waliofika kwenye mnada wa Itenge uliopo kwenye Kijiji cha Itenga A, Kata ya Itenga, Wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi ambapo aliendelea kuwasisitizi juu umuhimu wa uvalishaji hereni kwenye mifugo.

.............................................

Wafugaji wa mkoa wa Rukwa wameukubali utaratibu wa utambuzi wa mifugo kwa kutumia hereni za kielektroniki kwa kuwa utawasaidia kudhibiti wizi wa mifugo.

Haya yamesemwa wafugaji katika Kijiji cha Itenga A, Kata ya Itenga, Wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi wakati walipotembelewa na wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wataalam kutoka Mkoa wa Katavi kwa lengo la kutoa elimu juu ya umuhimu wa utambuzi wa mifugo kwa kutumia hereni za kielektroniki.

Magunano Isaka mmoja ya wafugaji waliofika kwenye mnada huo ameishukuru sana serikali kwa kuanzisha mfumo wa utambuzi wa mifugo kwa kutumia njia ya kielektroniki kwani wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya wizi ya mifugo.

Isaka amesema kuwa wafugaji mkoani Katavi wamepokea mfumo huo kwa kuwa utawasaidia kukabiliana na tatizo la wizi wa mifugo. Lakini pia mfumo huo wa hereni za kielektroniki utasaidia wafugaji kutambulika na kuwawezesha kuweza kubata bima na mikopo serikalini. Aidha, kupitia mfumo huu serikali itaweza kutambua mahitaji ya wafugaji kulingana na idadi ya mifugo waliyonayo hasa kwenye eneo la malisho.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Udhibiti wa Magonjwa yaenezwayo na Wadudu kutoka WMUV, Dkt. Benezeth Lutege amesema kuwa serikali imeanzisha suala la utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa mifugo kwa lengo la kuwasaidia wafugaji ili waweze kupata masoko ya ndani na nje ya nchi.

Utambuzi huu utawasaidia wafugaji kutambulika kwa maana ya umiliki wa mifugo, idadi na ubora wa mifugo yao, kitu ambacho kitawasaidia katika uuzaji wa mifugo pamoja na mazao yake.

Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Katavi, Nehemia James amesema kuwa kwa mkoa wa Katavi wamejipanga kuhakikisha kuwa mifugo yote inayoingia mkoani hapo inavalishwa hereni lakini pia udhibiti wa mifugo utaanzia kwenye masoko kwa maana ya kwamba mfugo hauweze kuuzwa au kuchinjwa pasipo kuwa na hereni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com