WAKULIMA PAWAGA WANUFAIKA NA TEKNOLOJIA YA KINYONGA



Picha ikionesha zao aina ya Nyanya, linalotumia kilimo cha umwagiliaji cha teknolojia ya kinyonga katika skimu ya Kiwere, iliyo katika Halmashuri ya wilaya ya Iringa
Mhandisi wa Umwagiliaji Mkoa wa Iringa Onesmo Kahogo akizungumza kuhusu teknolojia ya kilimo cha umwagiliaji maarufu kwa jina la Kinyonga.
Bw. Abdala Taveli Mkulima kutoka skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya Kiwere inayotumia Teknolojia ya Kinyonga, wilayani Iringa.
Zao aina ya Nyanya, linalotumia kilimo cha umwagiliaji cha teknolojia ya kinyonga katika skimu ya Kiwere, katika Halmashuri ya wilaya ya Iringa.
***
Na Mwandishi Wetu – Iringa

Wakulima katika skimu za kilimo cha umwagiliaji Kiwere na Mafuruto, wamenufaika na teknolojia ya kisasa katika sekta ya kilimo cha Umwagiliaji, ambayo ni mbadala wa matumizi ya rasilimali maji,maarufu kwa jina la kinyonga.

Mhandisi wa Umwagiliaji mkoani Iringa Onesmo Kahogo, amesema mwishoni mwa wiki mkoani Iringa kuwa, teknolojia hii inasaidia kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabianchi, kwani itamsaidia mkulima kupima kiwango cha maji anayohitaji kutumia shambani na haina madhara kwa mazao.

Mhandisi Kahogo amesema Teknolojia hii imesaidia kupungua migogoro ya maji kwa wakulima na inampa mkulima nafasi ya kufanya shughuli nyingine za uzalishaji.

Teknolojia hiyo inayotumia kifaa maalum kinachofukiwa ardhini ambacho, kinaruhusu eneo linalotumika kwa kilimo wa wakati huo kutumia maji yanayotosha kumwagiliwa katika eneo husika na kwa kiasi ambacho mkulima anakuwa amejipimia kulingana na mahitaji ya maji kwa wakati huo.

Kwa upande wake katibu wa skimu ya Kiwere maarufu kwa jina la Tupendane Bw. Abdalah Taveli, amesema teknolojia hiyo inasaidia kupata mazao mengi kwa kutumia maji kidogo akitolea mfano ya mavuno ya gunia sabini za vitunguu katika hekari moja.

Amesema pamoja na teknolojia hiyo kutumia maji kidogo inasaidia pia matumizi madogo ya pembejeo, kutokana na kwamba hazisombwi na maji shambani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post