Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANAOTUHUMIWA KUMUUA MWALIMU WAKAMATWA MUSOMA



JESHI la Polisi Mkoani Mara limefanya Operesheni maalumu kwenye Halmashauri zote na kukamata watuhumiwa 22 wakiwemo Wawili ambao wanahusishwa na mauaji ya Mwalimu Dickson James (27) wa Shule ya Msingi Busambara wilayani Musoma mkoani Mara.

Mwili wa James ulikutwa umetelekezwa mashambani, Disemba 7 Mwaka huu, majira ya saa 2 usiku katika Kitongoji cha Nyakato, Kijiji cha Nyang’oma huku mikono yake ikiwa imefungwa kwa kamba.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, SP Longinus Tibishubwamu, marehemu aliibiwa Pikipiki yake yenye Namba za usajili MC 179 CYQ aina ya Super Tiger.

Operesheni hiyo iliyoanza 26 Oktoba hadi 09 Disemba Mwaka huu majini na nchi kavu, imewezesha kukamatwa mali mbalimbali za wizi zikiwemo Pikipiki 12, Magodoro 11 likiwemo Moja la Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kwangwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com