Zaidi ya wanakwaya 20 wamefariki dunia, 10 wameokolewa baada ya basi kupinduka kwenye mto Mwingi nchini Kenya.
Katika video iliyoonekana na gazeti la Star leo siku ya Jumamosi Desemba 4,2021 ,basi hilo lilijaribu kuliongoza gari hilo kupita daraja lililofurika maji kwa usaidizi wa wakazi.
Baada ya dakika chache, basi hilo lilionekana likihangaika kusogeza magurudumu yake kwa vile mawimbi ya maji yalikuwa makali sana hivyo kulipeleka mtoni.
Kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Mashariki Joseph Yakan alithibitisha kisa hicho na kuongeza kuwa waumini wa Kanisa Katoliki la Mwingi walikuwa wakielekea harusini.
The Standard limeripoti kuwa basi hilo lilikuwa na takriban watu 30, ajali hiyo ilipotokea saa 11 asubuhi katika Kijiji cha Ngune, Mwingi ya Kati.
Polisi walisema wanakwaya hao walikuwa wakielekea kwenye harusi ya mwenzao.
Baadhi ya abiria walionekana wakipiga kelele na kuinua mikono yao kupitia madirishani huku basi hilo likizama taratibu.
Basi la abiria 51 la St Joseph Seminary Mwingi lilikuwa limebeba abiria 30 lilipozama kwenye mto uliofurika mwendo wa saa tano kando ya barabara ya Nguni-Nuu.
Yakan alisema waathiriwa ambao wengi wao walikuwa wanakwaya wa Kanisa Katoliki la Mwingi walikuwa wakielekea harusini eneo la Nuu.
Kwa mujibu wa video iliyochapishwa kwenye mtandao, dereva wa basi hilo alikuwa ameonywa dhidi ya kujaribu kuvuka mto huo.
"Nimemwambia asijaribu bana, basi si lori ...sasa ona ameua watu jameni. Basi hilo linaendelea kuzama na limejaa watu, wakiwamo watoto," mmoja wa mkazi anaskika akisema.
Dereva huyo alionekana akivuka daraja hilo lililofurika maji na baada ya sekunde kadhaa maji yakalishinda nguvu basi hilo.
Wakazi walikimbia kwenye eneo la mkasa na kuonekana kujaribu kuwaokoa waliokuwa ndani kabla ya basi kuishia majini.
Katika utabiri wake wa Novemba 30 hadi Desemba 6, 2021, idara hiyo ilisema kuwa wingu la mvua litazidi kushuhudiwa kuendelea katika maeneo kadhaa ya nchi.
Idara hiyo ilidokeza kwamba hali hiyo itashuhudiwa katika nyanda za juu mashariki mwa Bonde la Ufa, nyanda za chini kusini-mashariki na pwani.
Social Plugin