Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Magesa Mahona anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 60 na 65 mkazi wa mtaa wa Ugweto manispaa ya Shinyanga amefariki dunia kwa kujinyonga katika nyumba yake majira ya usiku.
Mwili wa marehemu uligunduliwa na familia yake leo asubuhi Jumamosi Januari 8,2022 baada ya kukutwa ukining’inia. Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, ACP George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Social Plugin