Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AUBAMEYANG KUTIMKIA BARCELONA



MUDA wowote kuanzia sasa, mshambualiaji wa Arsenal, Pierre-Emerick Emiliano François Aubameyang atajiunga na Barcelona kwa mkopo kabla ya dirisha la usajili halijafungwa usiku wa leo.

Video mbalimbali zimemuonyesha Aubameyang akiwa jiji la Barcelona tayari kujiunga na klabu hiyo baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Arsenal kutokana na masuala ya kinidhamu dhidi ya kocha wake Mikel Arteta.

Arsenal wameshangazwa na uamuzi huo wa ghafla ambao hawakuutarajia kwa Auba ambaye mara yake ya mwisho kuonekana uwanjani ilikuwa Desemba 6, mwaka jana akiitumikia Arsenal, aliiacha Timu yake Duabi mwezi ikiwa kambini.

Inaelezwa kuwa kabla dirisha la usajili halihafungwa hii leo, Auba anaweza kutangazwa kwani tayari makubaliano ya vilabu hivyo viwili yameshafikia mwafaka huku ikisalia makubaliano ya mshahara na Auba kiasi gani atalipwa.



Timu kama Juventus walikuwa wakimuwinda mshambuliaji huyo raia wa Gabon mwenye umri wa miaka 32 huku wakiweka mpango wa kumtoa kwa mkopo Alvaro Morata lakini ilishindikana. Kocha Xavi ameonyesha kuvutiwa na uwezo wa mkali huyo wa kufumania nyavu aliyekosana na Arteta kwa sababu za utovu wa nidhamu.



Dili hilo linachagizwa na fukuto la Osmane Dembele ambaye kocha Xavi amemtaka kutafuta timu nyingine huku akihusishwa kuelekea PSG ya Ufaransa. Auba yupo tayari kufanya vipimo leo na kuanza kuwatumikia miamba hao wa Hispania.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com