WATU tisa wamefariki dunia, na wengine sita wameokolewa wakiwa hai na wengine zaidi ya kumi hawajulikani walipo baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama baharini katika Mkoa wa Kusini Pemba, Visiwani Zanzibar, jana jioni Jumanne, Januari 4, 2022.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Richard Thadei Mchomvu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa watu hao wakitokea Chakechake kwenda msibani katika Kisiwa cha Panza lakini chanzo cha ajali akijajulikana mpaka sasa lakini boti lilikuwa na takribani watu 30 hadi 40.
“Nahodha hajapatikana na hali ya hewa haikuwa mbaya hivyo hatujajua chanzo kamili maana inaonekana tatizo sio upepo,” Kamanda Mchomvu alieleza na kuongeza kuwa zoezi la uokoaji litaendelea leo Jumatano asubuhi kufuatilia na jana zoezi lilisitishwa kwa sababu ya giza lakini ana hakika wote watapatikana wakiwa hai au vyovyote itakavyokuwa.
Social Plugin