SERIKALI ya Marekani imetoa wito wa kutaka kucheleweshwa kwa shughuli ya usambazaji wa mtandao wa kasi ya 5G kwenye simu za mkononi kutokana na uwezekano kuathiri usafiri wa anga.
Waziri wa Uchukuzi Pete Buttigieg na Mkuu wa Usimamizi wa Anga (FAA), Steve Dickson wametoa wito kwa waendeshaji wa mitandao wa AT&T na Verizon kuahirisha kwa wiki mbili uzinduzi wa mtandao huo uliopangwa kufanyika Januari 5.
FAA inahofia teknolojia ya 5G inaweza kuingilia utendaji kazi wa vifaa fulani vya kieletroniki vya ndege, na kuongeza kuwa masafa yanayotumika na mtandao wa 5G nchini Marekani yanakaribia kufanana na masafa yanayotumika katika altimita za ndege.