Gari linalopaa lenye uwezo wa kusafiri kilomita zaidi ya 160 kwa saa kwa na urefu wa zaidi ya mita 2,500 imepewa kibali kinachofaa kupaa na mamlaka ya usafiri ya Slovakia.
Ikiwa kama gari na ndege, AirCar ina injini ya BMW na hutumia petroli ya kawaida. Kampuni hiyo inasema kuwa imefanya safari za majaribio za saa 70 ili kupata cheti hicho, pamoja na zaidi ya safari za angani 200 na kutua.
Cheti cha “AirCar’ kinafungua milango ya uzalishaji mwingi wa magari yenye ufanisi wa juu zaidi yanayosafiri ,” alisema muasisi wake, Profesa Stephen Klein.
“Huu ni uthibitisho rasmi na wa mwisho wa uwezo wetu wa kubadilisha njia tunayosafiri safari za urefu wa masafa ya kati.”