Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KANISA LAPOROMOKA NA KUUA WAUMINI WAKIENDELEA NA IBADA YA SIKU 21 ZA KUOMBA NA KUFUNGA

Polisi katika jimbo la Delta kusini mwa Nigeria wamethibitisha kuwa watu watatu wamefariki kufuatia kuporomoka kwa jengo la kanisa la maarufu la lililopo katika mji mkuu wa jimbo, Asaba.

Polisi wa jimbo la Delta wameithibitishia BBC Idhaa ya Pidgin kuwa ‘’jana usiku wakati jingo hilo lilipoporomoka waliweza kuwaokoa watu 18, watatu wakiwa mahututi, lakini kufikia leo asubuhi watatu hao walithifitishwa kuwa wamefariki ."

Mkuu wa polisi DSP Edafe juhudi za uokozi zinaendelea katika eneo la tukio, zinazofanywa na huduma za dharura.

Alielezea kuwa kanisa hilo lilikuwa likiendesha ibada katika sehemu ya juu ya jingo, na kwahiyo sehemu ya juu haikuporomoka na hivyo kuwawezesha baadhi ya watu kutoka kutoka kwenye jingo hilo.

Tukio hilo lilitokea muda wa jioni Jumanne , na waandishi wa habari wanasema kanisa hilo lilikuwa likiendesha mpango wa ibada ya kilele cha siku 21 za kuomba na kufunga.

Matukio ya kuporomoka kwa majengo hutokea mara kwa mara nchini Nigeria

Vyombo vya nchini humo vinasema kanisa hilo lilikuwa likiendesha ibada ya siku 21 za kuomba na kufunga wakati jengo hilo liliporomoka.

Kwa sasa kanisa hilo linashirikiana na idara husika kufanya uchunguzi wa kubaini chanzo cha jengo hilo kuporomoka.

Chanzo - BBC Swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com