Mkuu wa Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga, Askofu Dkt. Emmanuel Joseph Makala (kushoto) akimtunuku Shahada ya Udaktari wa Falsafa Dkt. Kulwa Meshack wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga yamefanyika huku wanafunzi sita wakihitimu masomo ya dini ya Kikristo ya Theolojia katika ngazi ya Shahada (Bachelor), Umahiri (Master), na Ubobevu/Udaktari wa Falsafa (PhD).
Mahafali hayo ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon Kampasi ya Shinyanga kilichopo Ndala Mjini Shinyanga yamefanyika leo Ijumaa Januari 21,2022 katika ukumbi wa chuo cha Ualimu Shinyanga (SHY COM) ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Chuo (Chancellor) cha Therapon Dkt. Emmanuel Joseph Makala ambaye ni Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria.
Akiwatunuku vyeti, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga, Askofu Dkt. Emmanuel Joseph Makala amewaomba wananchi wachangamkie fursa zilizopo katika Chuo hicho cha mfano kinachopokea wanafunzi kutoka madhehebu yote ya dini.
“Wanaosoma hapa wakienda kwenye jamii matokeo makubwa yaonekane, Mitaala ya shule zetu ziwe za kiserikali, ziwe za kidini imekuwa nadharia sana kwa muda mrefu. Kwa hiyo nashukuru kusikia huu upekee uliopo katika chuo hiki iweze kuleta matunda makubwa hapa Shinyanga, hatuna vyuo vingi”, amesema Askofu Dkt. Makala.
“Katika upande wa Teolojia naomba mtuokoe, Chuo hiki kinapokea wanafunzi wa madhehebu yote. Katika kukua kwa kanisa Afrika kuna tatizo moja tu, Theolojia safi,naombeni sana mjikite kuliokoa kanisa hili linalokua sana Afrika. Pamoja na kukua kwa kanisa bado kuna shida katika Teolojia na mifano ipi mingi tu, Ushoga tumeukataa nina mashaka kama tumekaa kwa vitendo,kwa hiyo chuo hiki kiwe makini ili kuliokoa kanisa”,amesema Askofu Dkt. Makala.
“Kuna mambo ya Theolojia za kihuni huni mimi naona sehemu nyingi akina mama wanadhalilishwa,akina mama eti wanavuliwa nguo na Nabii, hilo siyo kanisa. Kuna makorokoro humo ndani ambayo hayavumiliki sasa huko siyo kuliokoa kanisa.
Kwa hiyo naombeni sana hata kama wakiwaambia mna mambo ya kale, shikeni neon la Mungu na msimamo wa Kikristo ili kanisa letu linapokua likue katika Teolojia safi.Tumieni fursa hii kuwafundisha watu mbalimbali namna ya kusaidia jamii ili tuondokane na skendo mbaya mbaya”, amesema Askofu Makala.
Akitoa Mahubiri wakati wa mahafali hayo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Therapon Mchungaji Masunga Ipimilo amewataka wananchi wa Shinyanga kuchangamkia fursa ya chuo hicho akieleza kuwa Therapon University wanaweza kuibadilisha kabisa Shinyanga.
“Huu ni mlango mwingine mmeletewa Shinyanga unaweza kuisaidia Shinyanga. Waungeni mkono Therapon University, nendeni mkasome ili mbadilishe jamii ya Shinyanga na nchi kwa ujumla. Tunakushukuru sana Baba Askofu Dkt. Emmanuel Makalla kwa kazi hii muhimu”,amesema Mchungaji Ipimilo.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Therapon tawi la Shinyanga, Mchungaji Dkt. Kulwa Meshack amesema chuo hicho kinatoa Kozi za pekee na kumwezesha mwanafunzi kusoma kwa njia ya mtandao akiwa akiwa nyumbani au kazini kwake.
“Sisi tuna Kozi za pekee sana zikiwemo za dini (Theolojia) kati ya Vyuo vyote chuo hiki ni the best of all. Tunakupa thamani ukiwa hapo nyumbani kwako, hapo hapo kazini kwako Presentation zinafanyika kwa njia ya mtandao. Kutokana na baadhi ya changamoto zilizojitokeza pia tuliamua tuwe tunakutana na wanafunzi wetu uso kwa uso kila baada ya siku 14, na baada ya siku hizo 14 wanaondoka na kazi za kufanya wakiwa kazini au nyumbani kwao”,amesema Dkt. Meshack.
“Chuo siyo majengo, programs zetu ni nzuri zipo Online. Tumejielekeza kwenye mambo ambayo ni changamoto kwenye maisha yetu ya kila kila siku. Tunakufundisha namna ya kufanya shughuli za kimaendeleo. Watu wengi wanafundisha uzushi, sisi tunataka watu wetu walielewe neno la Mungu kwa usahihi”,ameongeza Dkt. Meshack.
“Ada zetu ni nafuu sana. Chuo cha Therapon chenye makao makuu yake Texas Marekani kina wahadhiri wazuri waliobobea katika fani mbalimbali na tuna mahusiano na vyuo vingine na mahusiano yaliyopo baina ya mwanafunzi na mwalimu ni mazuri”,ameeleza.
Naye Mkuu wa Taaluma Chuo Kikuu cha Therapon Kampasi ya Shinyanga, Dkt. Emmanuel Buganga amezitaja kozi/programs zinazofundishwa Therapon University (Shinyanga Campus) kuwa ni Diploma (Stashahada), Bachelor (Shahada), Master (Umahiri) na Doctor (Udaktari) katika Nyanja 7 ambazo ni 1. Theology (theolojia) 2. Biblia (Biblical Studies) 3. Apologetics (Utetezi wa Imani) 4. Utawala na Uongozi Mkakati wa Taasisi (Leadership &Strategic Management) 5. Christian Counseling (Ushauri wa Kikristo 6. Christian Ministries (Huduma za Kikristo) 7. Chriatian Religious Education (Elimu ya Dini ya Kikristo Kikristo).
Dkt. Buganga amewakaribisha wanaopenda kujiunga na Chuo Kikuu cha Therapon wawasiliane na Viongozi wa Therapon University Kampasi ya Shinyanga Academic Dean Dr. Emmanuel Buganga kwa simu namba 0787699045, Email : emmanuelelias2005@yahoo.com au Vice Chancellor Dr. Kulwa Meshack simu namba 0755787127 au Email meshackkulwa@yahoo.com pia watembelee Tovuti ya Therapon University www.therapouniversity.org
ANGALIA PICHA MATUKIO WAKATI WA MAHAFALI HAPA CHINI
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga, Askofu Dkt. Emmanuel Joseph Makala akizungumza wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga yaliyofanyika leo Ijumaa Januari 21,2022. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Therapon tawi la Shinyanga, Mchungaji Dkt. Kulwa Meshack, kushoto ni Mkuu wa Taaluma Chuo Kikuu cha Therapon Kampasi ya Shinyanga, Dkt. Emmanuel Buganga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga, Askofu Dkt. Emmanuel Joseph Makala akizungumza wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga yaliyofanyika leo Ijumaa Januari 21,2022.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Therapon (Vice Chancellor) Kampasi ya Shinyanga, Mchungaji Dkt. Kulwa Meshack akizungumza wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga yaliyofanyika leo Ijumaa Januari 21,2022.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga, Askofu Dkt. Emmanuel Joseph Makala (katikati) akiwa amesimama na Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Therapon Kampasi ya Shinyanga wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga.
Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali yao ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga.
Mkuu wa Taaluma Chuo Kikuu cha Therapon Kampasi ya Shinyanga, Dkt. Emmanuel Buganga akizungumza kwenye Mahafali yao ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga, Askofu Dkt. Emmanuel Joseph Makala (kushoto) akimtunuku Shahada ya Theolojia Charles Mashenene wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga, Askofu Dkt. Emmanuel Joseph Makala (kushoto) akimtunuku Shahada ya Theolojia Enock Charles Lyeta wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga

Enock Charles Lyeta akionesha cheti chake wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga, Askofu Dkt. Emmanuel Joseph Makala (kushoto) akimtunuku Shahada ya Theolojia Malaki Joseph Bujiku wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga

Malaki Joseph Bujiku akionesha cheti chake wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga, Askofu Dkt. Emmanuel Joseph Makala (kushoto) akimtunuku Shahada ya Theolojia Obeid Fumbuka Jilala wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga

Obeid Fumbuka Jilala akionesha cheti chake wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga, Askofu Dkt. Emmanuel Joseph Makala (kushoto) akimtunuku Shahada ya Umahiri wa Theolojia Charles Petro Lugembe wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga

Charles Petro Lugembe akionesha cheti chake wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga, Askofu Dkt. Emmanuel Joseph Makala (kushoto) akisalimiana Dkt. Kulwa Meshack kabla ya kumtunuku Shahada ya Udaktari wa Falsafa wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga, Askofu Dkt. Emmanuel Joseph Makala (kushoto) akimtunuku Shahada ya Udaktari wa Falsafa Dkt. Kulwa Meshack wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga, Askofu Dkt. Emmanuel Joseph Makala (kushoto) akimtunuku Shahada ya Udaktari wa Falsafa Dkt. Kulwa Meshack wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga
Dkt. Kulwa Meshack akionesha cheti chake wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga.
Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali yao ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga, Askofu Dkt. Emmanuel Joseph Makala na Wahadhiri wakipiga picha ya kumbukumbu na Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali yao ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga, Askofu Dkt. Emmanuel Joseph Makala akiwafanyia maombi ya baraka Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali yao ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Therapon tawi la Shinyanga, Mchungaji Dkt. Kulwa Meshack akizungumza wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Therapon Mchungaji Masunga Ipimilo akihubiri kwenye Ibada wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Therapon Mchungaji Masunga Ipimilo akihubiri kwenye Ibada wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga
Mchungaji Joseph Bujiku akiongoza wimbo wa Tenzi kwenye Ibada wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga
Wanakwaya kutoka EAGT Lubaga Shinyanga wakiimba kwenye Ibada wakati wa Mahafali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga
Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Therapon Charles Mashenene akitoa ushuhuda jinsi chuo hicho kilivyomnufaisha
Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali yao ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali yao ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin