MCHUNGAJI Mkuu wa Kanisa la Olomore Abeokuta, Mchungaji Timothy Oluwatimilehin, amekamatwa na maafisa wa Polisi wa Ogun nchini Nigeria kwa madai ya kuwashawishi mama mwenye nyumba na binti zake wawili waache familia yao na aweze kulala nao akidai kashawishiwa na shetani.
Mume wa mwanamke huyo, ambaye hakuweza kumwokoa mkewe na binti zake wawili kutoka kwa Mchungaji Oluwatimehin kutokana na masuala hayo ya kimapenzi, alisaidiwa na maafisa wa idara ya Masuala ya Wanawake ya Ogun, ambao walishangazwa na madai ya kesi hiyo Kituo cha Polisi cha Adatan.
Msemaji wa Polisi wa Ogun Abimbola Oyeyemi aliyasema hayo kwa wanahabari siku ya Alhamisi.
Msemaji wa Polisi alisema kuwa mtuhumiwa alikiri kutenda kosa hilo; “Mchungaji amekiri kutendeka kwa uhalifu lakini akaomba msamaha. Katika ungamo lake, alieleza kuwa alichukua fursa ya kutokuelewana kati ya mwanamke huyo na mumewe kutekeleza kitendo hicho cha kishetani”.
“Kamishna wa Polisi, CP Lanre Bankole ameagiza kitengo cha kupambana na biashara haramu ya binadamu na utumikishwaji wa watoto cha Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai na Upelelezi wa Jimbo hilo kuisimamia kesi hiyo na kuichunguza kwa umakini kwa lengo la kumfikisha mahakamani mtuhumiwa haraka iwezekanavyo”.
Social Plugin