Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MREMBO ATOSWA BAADA KUMPA FIGO MPENZI WAKE




MWANADADA Colleen Le aliyempa mpenzi wake figo yake amedai kuwa jamaa huyo alitwaye Christian amempiga chini miezi saba tu kadhaa baada ya kujitoa kwake.

The Mirror imeripoti kuwa Colleen Le mwenye umri wa miaka 30, kutoka Marekani, alijitolea kumpa mpenzi wake figo yake moja baada ya kugundulika kuwa na maradhi mbaya ya figo.

Tatizo la figo zake lilianza alipokuwa na umri wa miaka 17, na aliarifiwa kwamba figo yake ingefanya kazi chini ya asilimia tano. Baada ya vipimo na kuona uwezekano wa kumpa, Colleen alitoa figo yake moja, na wote wawili wakapona kabisa.


Hata hivyo, uhusiano wao uliingia doa miezi saba baada ya upasuaji huo wakati Christian alisema anataka kuhudhuria sherehe ya watu makapera mjini Las Vegas pamoja na marafiki zake wa kanisa. Wakati aliporejea akitokea kwenye ziara hiyo, alikiri kwamba hakuwa mwaminifu kwake.

Alimsamehe lakini akamtema miezi mitatu baadaye; “Mabishano mengi baadaye, hatimaye nilimsamehe na kumpa nafasi ya pili. Ikiwa tumekusudiwa kila mmoja wetu, Mungu atatuleta pamoja mwishowe,” Colleen alisema. Video yake iliwavutia zaidi ya watu milioni mbili kwenye TikTok, huku wakimhurumia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com