Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANAFUNZI 10 BORA KWENYE MTIHANI WA KIDATO CHA PILI


Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) leo Jumamosi, Januari 15, 2022 limetangaza matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne uliofanyika Novemba 2021.

Matokeo hayo yametangazwa na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde ambapo pia, baraza hilo limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa kitaifa ya darasa la nne na kidato cha pili 2021.

Akitangaza matokeo hayo, Dkt. Msonde amesema watahiniwa wa Shule 422,388 (87.30%) kati ya Watahiniwa 483,820 wamefaulu Mitihani yao ongezeko la ufaulu ni 1.46% ikilinganishwa na mwaka 2020.

Watahiniwa 10 bora kwenye upimaji wa Wanafunzi wa kidato cha pili.
1. Geovin Macha – Shule ya Jude Arusha
2. Moses Masome – Heritage Pwani
3. Pius Tairo – Tengeru Arusha
4. Henry Shelembi -Jude Arusha
5. Shilanga Malegi – Heritage Pwani
6. Loi Kitundu – Feza Girls – DSM
7. Joshua Leo – Tengeru Boys Arusha
8. Brian Chille – Marian Mkoa wa Pwani
9. Cornel Karoli – Jude Arusha
10. Elizabeth Msengi – St. Monica Arusha.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com