Polisi wa Kaunti ya Murang’a nchini Kenya wanamshikilia mwanaume mwenye umri wa miaka 41 kwa kosa la kumuua mtoto wake wa kike (16) anayesoma form one baada ya kurudi nyumbani kwake na kumkuta mtoto wake huyo akiwa na mpenzi wake kitandani wakifanya mapenzi ndani ya nyumba ya baba yake.
Polisi wamesema Baba huyo alimpiga mtoto wake huyo aliyekuwa akisoma katika Shule ya Sekondari Sabasaba hadi akafariki na kutokana na hofu ya kukamatwa aliamua kuutupa mwili wa mtoto wake ndani ya karavati (Culvert) lililopo Barabara ya Kenol – Sabasaba umbali wa mita chache kutoka nyumbani kwake ambapo mwili huo ulionekana na Wapita njia.
Polisi wanasema walikuta damu kwenye suruali ya mwanaume huyo wakati wa upekuzi na walipombana akakiri kumuu mwanae huku akisema mpenzi wa mtoto wake waliyekuwa kitandani na mtoto wake alifanikiwa kukimbia.
Social Plugin