Binti mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Wendy mkazi wa Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro amemuua mama yake mzazi (Mama Ipepu) ambaye ni Nesi mstaafu wa Hospitali ya KCMC.
Jeshi la Polisi limeufukua mwili Januari 9, 2022 katika Kata ya Rau baada ya kumhoji binti huyo kwa zaidi ya wiki mbili na kukiri kumchinja mama yake kwa panga na kumfukia nyumbani kwao
Inaelezwa kuwa ni takriban mwaka sasa ndugu na majirani wamekuwa wakiulizia Mama huyo alipo na kupatiwa majibu na binti yake kuwa amesafiri kwenye matibabu nje ya Nchi
Social Plugin