Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa wa Mbeya (Mbeya Press Club) Festo Sikagonamo Mwakasege amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Ijumaa Januari 07, 2022 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.
Taarifa hizo zimethibitishwa na Katibu wa Mbeya Press Club Keneth Mwakandyali.
Festo Sikagonamo amefanya kazi kwenye vyombo vya habari mbalimbali vya habari ikiwemo TBC na hadi kwenye nyanja ya uongozi alipokuwa Mwenyekiti wa Mbeya Press Club na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimisha.
R.I.P Festo Sikagonamo.
Social Plugin