Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWILI WA ASKARI ALIYEMPIGA RISASI MPENZI WAKE WAKUTWA UKIELEA MTONI



OFISA wa Polisi, David Nyanweya (28) ambaye alimpiga risasi mara sita Mpenzi wake Everlyne Njoki, tarehe 22 Agosti, 2020 baada ya kugombana wakiwa nje ya Kituo cha Polisi cha Laare Kaunti ya Meru nchini Kenya amekutwa amefariki huku mwili wake ukielekea katika Mto Kathitha.

Mwili wake ulibainika na watu ambao walikuwa Picnic ambao walitoa taarifa Polisi ambao wamesema bado wanachunguza kama amejiua au ameuawa na mwili wake kutupwa Mtoni “Huenda Mpenzi wake ambaye alinusurika kuuawa kwa risasi akahojiwa ili tujue kama amelipiza kisasi ama laah”

Licha ya kupigwa risasi sita Everlyne alipona baada ya madaktari kusema risasi hizo hazikuathiri maeneo nyeti na baada ya kutoka Hospitali alitangaza kuwa amemsamehe Askari huyo na hana kinyongo kabisa ingawa alisema anaendelea na maisha yake na hataki tena kuendelea na mapenzi yao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com