Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NANCY FOUNDATION YASHEREHEKEA MWAKA MPYA 2022 NA AKINA MAMA WALIOJIFUNGUA KITUO CHA AFYA BUGISI...YAMWAGIWA SIFA KUOKOA MAMA NA MTOTO

Msimamizi wa Kituo cha Afya Bugisi Sister Kathleen Costigan (katikati) akiongoza zoezi la kukata keki iliyoandaliwa na Asasi ya Nancy Foundation kwa ajili ya akina mama waliojifungua katika kituo cha afya Bugisi

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Idadi ya akina mama wanaojifungua katika Kituo cha Afya Bugisi kilichopo kwenye kijiji cha Chembeli kata ya Didia wilaya ya Shiyanga imekuwa ikiongezeka kila mwezi kutokana na motisha na huduma ya afya ya mama na mtoto inayotolewa na Asasi ya Marafiki Nancy Foundation.

Hayo yamebainishwa leo Jumamosi Januari 22,2022 na Mkuu wa Kitengo cha Mama, Baba na Mtoto katika Kituo cha Afya Bugisi Dkt. William Zakayo wakati Nancy Foundation ilipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya 2022 na kukutana na akina mama wanufaika wa huduma za afya zinazotolewa na Nancy Foundation.

Huduma zinazotolewa na Nancy Foundation katika kituo cha afya Bugisi ni virutubisho muhimu kwa mama na mtoto wakati wa ujauzito, Huduma ya Kioo (Utra Sound) kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya ujauzito na kuweza kutambua matatizo yanayohusiana na ujauzito pamoja na kutoa motisha ya Khanga kwa akina mama wanaojifungua ili kuhamasisha akina mama kujifungua katika kituo cha afya Bugisi kwa lengo la kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Akielezea mafanikio yaliyofikiwa katika kitengo cha Mama, Baba na Mtoto, Dkt. Zakayo amesema kumekuwa na mwitikio mzuri kwa akina mama kufika katika kituo cha afya Bugisi kupata huduma za afya.

“Nancy Foundation mmeleta chachu na hamasa kwa akina mama wanaofika kupata huduma za afya. Mmetufanya tutambulike kwa huduma zetu.Tunapokea wateja wengi kutoka maeneo ya vijijini wanaokuja kuanza huduma na kujifungua hapa”,amesema Dkt. Zakayo.

Dkt. Zakayo amesema kabla ya Nancy Foundation kuanza kutoa huduma mwaka 2017 katika kituo cha afya Bugisi walikuwa wanapokea akina mama 30 hadi 35 kwa mwezi waliokuwa wanafika kupata huduma ya mama na mtoto lakini hivi sasa kuna ongezeko kubwa hadi kufikia akina mama 60 hadi 85 kwa mwezi mmoja.

Kwa upande wa akina mama wajawazito awali walikuwa wanapokea akina mama 50 hadi 60 kwa mwezi lakini sasa wanapokea kuanzia 70 hadi 80 wakati mwingine 100 kwa mwezi mmoja kutokana na huduma bora na huduma bure ikiwemo Utra Sound na Khanga zinazotolewa katika kituo cha afya Bugisi.

“Kutokana na virutubisho muhimu kwa mama na mtoto wakati wa ujauzito vinavyotolewa na Nancy Foundation akina mama wajawazito wanaohudumiwa hapa hawapati changamoto ya upungufu wa damu na wanapatiwa huduma bora za afya”,ameongeza Dkt. Zakayo.

Kwa upande wake, Msimamizi wa Kituo cha Afya Bugisi Sister Kathleen Costigan ameishukuru asasi ya Nancy Foundation kwa msaada inaotoa kwa akina mama wanaofika katika kituo hicho cha afya ikiwemo kuwapatia hamasa ya Khanga akina mama wanaojifungua,huduma ya Utra Sound na virutubisho muhimu kwa mama na mtoto wakati wa ujauzito.

Kathleen ametumia fursa hiyo kuwahamasisha akina mama kufika katika kituo cha afya Bugisi kwani wanatoa huduma bora za afya hivyo waepuke tabia ya kujifungulia nyumbani ili kuepuka vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na uzazi.

“Tunawakaribisha wananchi kuja kupata huduma za afya hapa kwani furaha yetu ni kuhudumia wagonjwa. Huduma zetu ni bure na zingine tunatoa kwa gharama nafuu sana ukilinganisha na hospitali zingine. Hivi karibuni tutaanza kutoa huduma za upasuaji ‘Theatre’ hali itakayosaidia kupunguza idadi ya wagonjwa tunaowapa rufaa kwenda hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga”,ameongeza Kathleen.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa asasi ya Marafiki Nancy Foundation nchini Tanzania, Ezra Manjerenga amesema Asasi hiyo inayoundwa na marafiki kutoka Tanzania na Marekani, inajihusisha na huduma ya afya ya mama na mtoto na ilianza kutoa huduma katika kituo cha afya Bugisi Agosti mwaka 2017.

“Tumefika hapa kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya 2022 na kukutana na akina mama wanufaika wa huduma zinazotolewa na Nancy Foundation katika kituo cha afya Bugisi.

Tumefarijika kuona idadi ya akina mama wanaofika katika kituo cha afya kupata huduma za afya na kuachana na tabia ya kujifungulia nyumbani hali ambayo inachangia vifo vya mama na mtoto”,amesema Manjerenga.

“Nancy Foundation imetokana na Mtoto Nancy ambaye alizaliwa njiti ‘Pre mature’ kutokana na changamoto za uzazi hivyo marafiki wakaamua kutumia changamoto alizopitia mtoto huyo na kuanzisha huduma za kujitolea kwa ajili ya kuchangia huduma ya mama na mtoto katika kituo cha afya Bugisi kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga”,amesema Manjerenga.

Naye Dkt. Justice Minofu kutoka Shirika la Doctors With Africa,ambaye ni miongoni mwa marafiki wa Nancy Foundation amewashauri akina mama kuachana na tabia ya kujifungulia nyumbani kwani inahatarisha maisha ya mama na mtoto akisisitiza kuwa huduma bora za afya zinapatikana hospitali pekee.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji wa kata ya Didia Jackson Maganga ameiomba Nancy Foundation kuendelea kukisaidia kituo cha afya Bugisi kwani kimeleta manufaa makubwa ikiwemo kupunguza idadi ya akina mama wanaojifungulia nyumbani huku akiwaomba akina mama wanufaika wa huduma za Nancy Foundation kuwa Mabalozi na kuhamasisha akina mama kujifungulia kwenye vituo vya afya.

Nao baadhi ya akina mama akiwemo Esther Salu, Sophia Jisinza na Thereza Lutonja wameishukuru asasi ya Nancy Foundation na Kituo cha afya Bugisi kwa huduma bora wanazotoa kwa akina mama na watoto pamoja na wagonjwa wengine na kuahidi kuhamasisha akina mama kujifungulia kwenye vituo vya afya ili kuokoa uhai wa mama na mtoto.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mwakilishi wa asasi ya Marafiki Nancy Foundation nchini Tanzania, Ezra Manjerenga akiwa amebeba mtoto mchanga aliyezaliwa katika Kituo cha Afya Bugisi kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga . Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwakilishi wa asasi ya Marafiki Nancy Foundation nchini Tanzania, Ezra Manjerenga akiwa amebeba mtoto mchanga aliyezaliwa katika Kituo cha Afya Bugisi kilichopo katika wilaya ya Shinyanga wakati Nancy Foundation ilipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya 2022 na kukutana na akina mama wanufaika wa huduma za afya zinazotolewa na Nancy Foundation. Kulia ni mtoto Nancy ambaye ndiyo chimbuko la Asasi hiyo kwani alizaliwa njiti ‘Pre mature’ kutokana na changamoto za uzazi hivyo marafiki wakaamua kutumia changamoto alizopitia mtoto huyo na kuanzisha huduma za kujitolea kwa ajili ya kuchangia huduma ya mama na mtoto katika kituo cha afya Bugisi.
Msimamizi wa Kituo cha Afya Bugisi Sister Kathleen Costigan (katikati) akiongoza zoezi la kukata keki iliyoandaliwa na Asasi ya Nancy Foundation kwa ajili ya akina mama waliojifungua katika kituo cha afya Bugisi ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Mwaka Mpya 2022.
Msimamizi wa Kituo cha Afya Bugisi Sister Kathleen Costigan (katikati) akiongoza zoezi la kukata keki iliyoandaliwa na Asasi ya Nancy Foundation kwa ajili ya akina mama waliojifungua katika kituo cha afya Bugisi ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Mwaka Mpya 2022.
Mtoto Nancy ambaye ndiyo chimbuko la Asasi ya Marafiki Nancy Foundation akimlisha keki Msimamizi wa Kituo cha Afya Bugisi Sister Kathleen Costigan. Kushoto ni Mwakilishi wa asasi ya Marafiki Nancy Foundation nchini Tanzania, Ezra Manjerenga.
Msimamizi wa Kituo cha Afya Bugisi Sister Kathleen Costigan (kulia) akimlisha keki Mtoto Nancy ambaye ndiyo chimbuko la Asasi ya Marafiki Nancy Foundation. Kushoto ni Mwakilishi wa asasi ya Marafiki Nancy Foundation nchini Tanzania, Ezra Manjerenga.
Mtoto Nancy ambaye ndiyo chimbuko la Asasi ya Marafiki Nancy Foundation akimlisha keki mmoja wa akina mama waliofika kupata huduma ya mama na mtoto katika kituo cha afya Bugisi. Kushoto ni Mwakilishi wa asasi ya Marafiki Nancy Foundation nchini Tanzania, Ezra Manjerenga.
Mwakilishi wa asasi ya Marafiki Nancy Foundation nchini Tanzania, Ezra Manjerenga akimlisha keki mmoja wa akina mama waliojifungua katika kituo cha afya Bugisi. Kulia ni Msimamizi wa Kituo cha Afya Bugisi Sister Kathleen Costigan.
Mwakilishi wa asasi ya Marafiki Nancy Foundation nchini Tanzania, Ezra Manjerenga akimlisha keki mmoja wa akina mama waliojifungua katika kituo cha afya Bugisi
Mwakilishi wa asasi ya Marafiki Nancy Foundation nchini Tanzania, Ezra Manjerenga akimlisha keki mmoja wa akina mama waliojifungua katika kituo cha afya Bugisi.
Mwakilishi wa asasi ya Marafiki Nancy Foundation nchini Tanzania, Ezra Manjerenga akimlisha keki mmoja wa akina mama waliojifungua katika kituo cha afya Bugisi
Mwakilishi wa asasi ya Marafiki Nancy Foundation nchini Tanzania, Ezra Manjerenga (kulia) akizungumza na akina mama katika kituo cha afya Bugisi wakati Nancy Foundation ilipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya 2022 na kukutana na akina mama wanufaika wa huduma za afya zinazotolewa na Nancy Foundation.
Mwakilishi wa asasi ya Marafiki Nancy Foundation nchini Tanzania, Ezra Manjerenga (katikati) akizungumza na akina mama katika kituo cha afya Bugisi wakati Nancy Foundation ilipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya 2022 na kukutana na akina mama wanufaika wa huduma za afya zinazotolewa na Nancy Foundation.
Mwakilishi wa asasi ya Marafiki Nancy Foundation nchini Tanzania, Ezra Manjerenga (kulia) akizungumza na akina mama katika kituo cha afya Bugisi wakati Nancy Foundation ilipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya 2022 na kukutana na akina mama wanufaika wa huduma za afya zinazotolewa na Nancy Foundation.
Afisa Mtendaji wa kata ya Didia Jackson Maganga (kulia) akizungumza wakati Nancy Foundation ilipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya 2022 na kukutana na akina mama wanufaika wa huduma za afya zinazotolewa na Nancy Foundation.
Dkt. Justice Minofu kutoka Shirika la Doctors With Africa,ambaye ni miongoni mwa marafiki wa Nancy Foundation akizungumza wakati Nancy Foundation ilipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya 2022 na kukutana na akina mama wanufaika wa huduma za afya zinazotolewa na Nancy Foundation.
Mkuu wa Kitengo cha Mama, Baba na Mtoto katika Kituo cha Afya Bugisi Dkt. William Zakayo akizungumza wakati Nancy Foundation ilipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya 2022 na kukutana na akina mama wanufaika wa huduma za afya zinazotolewa na Nancy Foundation.
Msimamizi wa Kituo cha Afya Bugisi Sister Kathleen Costigan (kulia) akizungumza wakati Nancy Foundation ilipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya 2022 na kukutana na akina mama wanufaika wa huduma za afya zinazotolewa na Nancy Foundation.
Esther Salu akiishukuru asasi ya Nancy Foundation na Kituo cha afya Bugisi kwa huduma bora wanazotoa kwa akina mama na watoto
Sophia Jisinza akiishukuru asasi ya Nancy Foundation na Kituo cha afya Bugisi kwa huduma bora wanazotoa kwa akina mama na watoto
Thereza Lutonja akiishukuru asasi ya Nancy Foundation na Kituo cha afya Bugisi kwa huduma bora wanazotoa kwa akina mama na watoto
Shamra shamra zikiendelea wakati wa zoezi la ukataji keki iliyoandaliwa na Nancy Foundation katika kituo cha afya Bugisi.
Shamra shamra zikiendelea wakati wa zoezi la ukataji keki iliyoandaliwa na Nancy Foundation katika kituo cha afya Bugisi.
Shamra shamra zikiendelea wakati wa zoezi la ukataji keki iliyoandaliwa na Nancy Foundation katika kituo cha afya Bugisi.
Moja ya mabango katika kituo cha afya Bugisi.
Mwakilishi wa asasi ya Marafiki Nancy Foundation nchini Tanzania, Ezra Manjerenga (wa pili kulia) na viongozi mbalimbali wakiondoka katika kituo cha afya Bugisi. Kushoto ni Msimamizi wa Kituo cha Afya Bugisi Sister Kathleen Costigan.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com