Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko Madogo katika Baraza la Mawaziri, Makatibu Wakuu, Manaibu Makatibu Wakuu.
Akitangaza mabadiliko hayo leo Jumamosi Januari 8, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amesema Rais Samia amefanya mabadiliko ya muundo katika Wizara tatu.
Mawaziri wapya watano walioteuliwa ni Nape Nnauye (Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari), Hamad Masauni (Mambo ya Ndani), Dk Pindi Chana (Sera Bunge na Uratibu), Anjelina Mabula (Ardhi) na Husein Bashe (Kilimo).
Rais Samia pia ameteua manaibu waziri wapya katika wizara tano.
Manaibu waziri hao wapya walioteuliwa ni pamoja na Anthony Mavunde (Kilimo), Jumanne Sagini (Mambo ya Ndani) Dkt. Lemomo Kiruswa (Madini), Ridhiwani Kikwete (Ardhi) na Atupele Mwakibete (Ujenzi na Uchukuzi).
Rais Samia ''ameunganisha wizara tatu, iliyokuwa wizara ya uwekezaji iliyokuwa chini ya ofisi ya Waziri Mkuu na pia ameunganisha wizara ya biashara moja ambayo itaitwa uwekezaji , viwanda na biashara'', amesema Balozi Hussein Kattanga.
Aidha kama alivyoahidi Rais Samia ameunda Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia ,wanawake na Makundi maalum.
Kilichojitokeza zaidi katika mabadiliko baraza la mawaziri yaliyofanywa na Rais Samia ni kuundwa kwa Wizara Mpya ambayo ni Wizara maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum, wizara hii itaaongoozwa na Waziri Dorothy Gwajima ambaye alikuwa waziri wa Afya.
Majina mapya yaliyoingia katika wizara ni pamoja na ya mawaziri kamili Nape Nnauye, Pindi Chana na Hamad Masauni, Angelina Mabula na Hussein Bashe.
Kwa upande wa manaibu Ridhiwani Kikwete ameteuliwa kuwa Naibu waziri wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi. Antony Mavunde Naibu wizara ya kilimo, Jumanne Sagini Naibu waziri wizara ya mambo ya ndani, Lemomo Kiruswa ambaye ni naibu waziri wa Madini, na Atupele Mwakibete naibu waziri wizara ya ujenzi na uchukuzi.
Samia amemteua Dkt.Francis K.Michael, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utali.
Pili, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Adolf H.Ndunguru, Naibu Katibu Mkuu (Sera), Wizara ya Fedha kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Madini;
Tatu, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Prof.Jamal A.Katundu, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu).
Nne, Mheshimiwa Rais Samia amemteua, Dkt.Jim J.Yonazi, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Tano, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Balozi Mhandisi Aisha S. Amour aliyekuwa Balozi Kuwait kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi).
Sita, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Profesa Eliamani M. Sedoyeka, Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Saba, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Mhandisi Felshesmi J.Mramba, Kamishina wa Nishati kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati.
Tazama Video Hapa chini
Social Plugin