MREMBO Stephanie Matto (31) aliyejiajiri kwa kujamba, kuufunga ushuzi na kuuza kwenye chupa na majagi ameamua kustaafu baada ya kukumbwa na balaa zito akiwa kazini.
Kwa mujibu wa New York Post, mrembo huyo juzi kati alilazwa baada ya kukimbizwa hospitalini kwa maumivu ya kifua baada ya gesi kumzidia tumboni akiwa kwenye harakati za kunywa supu ya maharage. Mwadada huyo amesema aliogopa sana akadhani labda kapatwa na kiharusi na huo ndio mwisho wake.
Mrembo huyo alikuwa akipendelea kula sana maharage, mayai na baadaye kuongeza protein shakes katika mchanganyiko wa msosi wake baada ya kuona inaongeza harufu mbaya katika mashuzi anayotoa kwa wateja wake.
Gesi kujaa tumboni kutokana na vyakula anavyokula ndio ikaanza kumletea shida ikabidi apige simu kwa rafiki yake amsaidie kumkimbiza hospitali na sasa ameamua kustaafu.
Familia yake imefurahia maamuzi yake hayo ya kustaafu na anamini hata sehemu zake husika zitakuwa zimefurahi kupumzishwa baada ya kazi hiyo nzito ya kusukuma bidhaa kila siku.
Mrembo huyo alianza biashara ya kujamba November 2021 ambapo kama utani akaanza kupata wateja mitandaoni waliokuwa wakinunua bidhaa hiyo aliyoifunga kwenye chupa na majagi.
Chupa moja aliweza kuuza kwa dola $1000 ambazo ni sawa na milioni 2.3 za Kibongo. Kipindi cha kuelekea msimu wa sikukuu alifanya punguzo maalumu kwa asilimia 50% ambapo wateja walizidi kumiminika kuhitaji bidhaa husika.
Kwa wiki aliweza kuuza hadi chupa 50 zilizojaa bidhaa hiyo sababu alirekebisha diet yake akawa anakula vyakula vya kumzidishia ongezeko la mashuzi yenye viwango na ubora ili kukabiliana na ushindani sokoni.
Mpaka sasa baada ya kuamua kustaafu ameweza kuingiza dola $200,000 ambazo ni zaidi ya milioni 461.2 za Kibongo. Biashara hiyo ya kujamba imeweza kumpa umaarufu haraka nchi nyingi ingawa mrembo huyo alianza kujulikana kupitia kipindi cha 90 Day Fiance.
Social Plugin