Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Simba SC Ahmed Ally, amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya kupata wadhifa huo. Ahmed ameonesha furaha yake na tayari yuko njiani kuelekea Zanzibar kuungana na kikosi kwenye Mapinduzi Cup.
Alichokisema Ahmed; “Nimeipokea nafasi hii kwa uzito wa Dunia Nzima, ni habari njema, ni habari kubwa, ni habari nzuri kweli kweli, ni ndoto imetimia ya kwenda kufanya kazi ndani ya Simba SC, kwa hiyo uzito wa habari hii unaweza kusema ni uzito wa Dunia Nzima.
“Naimani mimi ni chaguo sahihi kwa klabu ya Simba na ndio maana mchakato wa kumtangaza Afisa Habari wa Simba SC ulikua mrefu, hii ilimaanisha Uongozi ulikua unatafuta mtu sahihi na mkweli na awe Simba SC,” amesema Ahmed Ally.
Social Plugin