Kane Tanaka, mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani, alifikisha umri wa miaka 119 Jumapili, kwa mujibu wa ujumbe wa Twitter uliochapishwa na mjukuu wake wa kike, Junko Tanaka.
“Ni mafanikio makubwa. (Kane Tanaka) kufikisha umri wa miaka 119,” Junko aliandika kwenye tweeter, akiwa na picha ya bibi yake, ambaye alimwona mwezi Disemba. “Natumani utaendelea kuishi maisha kwa furaha na kwa ukamilifu.”
Junko alishirikisha picha kwenye Twitter ya chupa mbili za ukumbusho za Coca-Cola ambazo Tanaka alipewa katika siku yake ya kuzaliwa, zenye lebo zilizoonesha umri wake.
“Zawadi ya siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa 1: Natambulisha zawadi ambazo Kane amepokea.tumefurahia sana zawadi hii. Kampuni ya Coca-Cola ilitengeneza chupa ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa ajili yake. Inaonekana (Kane) bado anakunywa Coca-Cola kama kawaida,” Junko aliandika kwenye tweeter.
Kane alizaliwa mwaka 1903, na kuolewa na muuza duka la mchele akiwa na miaka 19,na alifanya kazi katika duka hilo la familia mpaka alipofikia umri wa miaka 103.
Social Plugin