Na Dinna Maningo, Tarime.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tarime kimedhamiria kujenga jengo la Ghorofa tano au nane kama kitega uchumi, litakalogharimu zaidi ya Bilioni moja ambapo hadi sasa tayari michoro imechukuliwa na kupelekwa makao makuu ya chama ili kupitiwa.
Akizungumza na Malunde 1 blog Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tarime ameeleza mbinu zitakazotumika kupata fedha za ujenzi,Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tarime Valentine Maganga alisema kuwa watatumia kiasi cha fedha zitokanazo na miradi ya chama na michango ya wadau wa maendeleo.
"Tunatarajia kujenga jengo la kitega uchumi la ghorofa kati ya tano hadi nane kutegemea na fedha,litajengwa kwa miaka kati ya mitatu hadi mitano,likikamilika tutapata wawekezaki kama wa benki,maduka na biashara zinginezo,tayari michoro imeshapelekwa makao makuu ya chama wapitie wakiturejeshea chama kitakaa kitasema kina sh.ngapi kisha wadau nao watachanga kwa hiari.
" Kama ni wafadhili watatuambia kiasi watakachotoa halafu baada ya ujenzi kukamilika atapewa chumba cha biashara atakuwa anakatwa kidogo kidogo hadi deni liishe na bahati nzuri tumepata wawekezaji watatu wameahidi kila mmoja kutoa milioni 50" amesema Maganga.
Maganga amesema kuwa CCM Tarime ina miradi inayowapatia fedha ambazo zimekisaidia chama kujiendesha, miradi hiyo ni ada za uanachama,kodi za vibanda na maduka 70 yaliyopo maeneo mbalimbali ndani ya wilaya hiyo ambapo kila mwaka ukusanya fedha zaidi ya milioni 100.
Ameongeza kuwa chama kina viwanja vinne,matawi yote ya chama katika wilaya hiyo yana ofisi,kuna ofisi za kata za kichama zipatazo 33 ambapo kata mbili ya Kiterere na Kata ya Sabasaba ndiyo hazina ofisi.
Mkazi wa kata ya Nkende Macheda Federico anasema kuwa kuna haja ya chama hicho kuanzisha mradi wa duka la kuuza mavazi ya chama kwakuwa Tarime hakuna duka linalouza nguo na bidhaa mbalimbali za chama.
"Hapa Tarime hakuna sehemu ya kupata vitu vya chama hakuna duka linalouza nguo za chama,mfano sasa hivi tunajiandaa kusherekea kuzaliwa kwa CCM anakuja Rais wanachama lazima tuvae sare za chama lakini hupati zinauzwa tu pale yanapotokea matukio ndiyo anajitokeza mtu mmoja anafata nguo Dar es salaam anakuja kutuuzia" anasema Federico.
Waitara Kemo mkazi wa Tarime mjini anasema kuwa chama cha CCM nisawa na zilivyo Taasisi zingine ni lazima kiwe na vyanzo vya mapato mbali na kutegemea michango ya wanachama,kuwa na miradi kama vile shule, Hoteli,Vyuo vya mafunzo mbalimbali ambapo mapato yake yatakiwezesha kujitegemea katika shughuli zake za cham
Social Plugin