RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameonyesha kukerwa na kile alichokisema Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu Serikali kukopakopa badala ya kujiendesha kwa pesa za ndani.
Samia amesema hayo leo Jumanne, Januari 4, 2022 wakati akipokea ripoti ya matumizi ya Fedha za Maendeleo (Fedha za Uviko-19), Ikulu jijini Dar es Salaam.
“Mtu mmoja aliniambia, atakayekusumbua kwenye uongozi wako ni shati ya kijani mwenzio (yaani Mwana-CCM) na sio mpinzani, mpinzani atakutazama unafanya nini, ukimaliza hoja zao hawana maneno, anayetazama mbele 2025 huyu ndiyo atakayekusumbua ndicho kinachotokea.
“Huwezi kufikiria mtu mliyemuamini, mshika mhimili, aende akasimame aseme yale. Ni stress ya 2025.
“Wakati mmenikabidhi huu mzigo, nilianza kusikia lugha zinasema serikali ya mpito, serikali ya mpito Bungeni huko kwa kina Kassim, nikarudi kwenye Katiba kuangalia serikali ya mpito imeandikwa wapi, sikuona, nikasema anhaa, twendeni,” Rais Samia.