Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHENGE AJITOSA KUFUKUZIA USPIKA WA BUNGE



MBUNGE wa Zamani wa Bariadi Magharibi (CCM) Andrew Chenge amejitosa katika kinyang’anyilo cha kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri kupitia Chama cha Mapinduzi.

Chenge aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mwenyekiti wa Bunge ameonesha nia ya kupanda ngazi ili kufikia nafasi ya juu ya uongozi wa Bunge hilo.

Baadhi ya Vigogo waliochukua fomu kipitia CCM ni pamoja na Naibu Spika wa sasa Dk Tulia Akson, Makamu wa Rais wa zamani wa Bunge la Afrika Stephen Masele, Waziri wa zamani katika Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mussa Azzan Zungu, Mbunge wa Geita Vijijini, Jeseph Kasheku Msukuma na wengine wengi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com