Kampuni ya kuunda magari kutoka nchini Ujerumani ya Mercedes – Benz, imezindua gari jipya linalotumia nishati ya umeme peke yake lililopewa jina la EQXX, ambapo gari hilo lina uwezo wa kutembea umbali wa maili 620, baada ya kuongezewa nguvu ya betri yake.
Aidha Kampuni ya Mercedes Benz imeongeza ubunifu katika gari hilo kwa kuweka paneli za jua kwenye paa la gari, ili kusaidia kuiongezea nguvu betri yake.
Gari hilo la kifahari limetengenezwa kwa ubunifu wa hali ya juu, kwa kutumia malighafi zinazoweza kurejereshwa (recycled) baada ya matumizi ya awali.
Kampuni hiyo Mercedes – Benz inakusudia ifikapo mwaka 2025, nusu ya mauzo ya magari yake yawe ni yale yanayotumia nishati ya umeme.
Social Plugin