NA
MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM
Mtandao
wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umemuomba Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan kuwapa nafasi na kuwasikiliza wananchi
wa Loliondo ili kusikia hoja zao na hatimaye azifanyie kazi ili kumaliza
mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu.
Kauli
hiyo imetolea leo Jijini Dar es salaam na Mratibu wa Kitaifa wa THRDC Onesmo
Olengurumwa wakati akizungumza na wanahabari akitoa taarifa ya hali ya utetezi
wa Haki za Binadamu katika migogoro ya Ardhi Wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Olengurumwa
amesema Wilaya ya Ngorongoro ina jumla ya Kilomita za mraba zaidi ya 14,ambapo
zaidi ya asilimia 75% ya eneo hilo kwa sasa hutumika kwa shughuli za utalii na
uhifadhi lakini pia kilomita za mraba 4000 kwa sasa zimebaki kwa matumizi ya
makazi ya watu na shughuli za kijamii.
‘Taharuki
imekuwa ikiibuka mara kwa mara katika kipindi cha miaka toka mwaka 1992 matukio
ya kuhamishwa watu yamekuwa yakifanyika mara ka mara na huku ukiukwaji wa haki
za binadamu ukishuhudiwa hivyo kwa sasa tunaamini Mhe Rais Samia akitoa nafasi
ya kuwasikiliza wananchi wa Ngorongoro huenda akawa ni wa kwanza kupatia
ufumbuzi wa kudumu migogoro ya ardhi na uhifadhi Wilayani Ngorongoro’amesema
Olengurumwa
Aidha
ameiomba serikali kusitisha mpango wake wa kuchukua ardhi za vijiji na badala
yake ikae na wananchi ili kutafuta suluhu itakayokubaliwa na pande zote.
Vilevile
ameiomba Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora kufanya uchunguzi kuhusu
malalamiko ya wananchi na kuchukua hatua stahiki ili kuzuia ukiukwaji wa haki
za binadamu Wilayani Ngorongoro.
Katika
hatua nyingine amewataka wananchi wa Loliondo kuwa tayari kukaa mezani kwa
lengo la kujadili suluhu ya kudumu kwa manufaa ya pande zote mbili ikiwa ni
pamoja na haki zao pamoja nha shughuli za uhifadhi kwa maslahi ya Taifa.
Akizungumzia
kuhusu ushiriki wa Watetezi wa Haki za Binadamu na Azaki wa Haki za wafugaji Wakili
kutoka THRDC Lulu Maro amesema kuwa wanasikitiswa na ushiriki mdogo wa
mashirika ya haki za binadamu katika kufanya utetezi kuhusuana na mgogoro huo
na hivyo kufanya haki za wananchi kupotea ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Amesema
ni vyema viongozi wa juu wa serikali wakaacha kukaa kimya badala yake wafanye
jitihada za kuwasikiliza wananchi wa Loliondo,Ngorongoro ili kuwafanya wananchi
wasiichi maisha ya hofu muda wote.
Hata hivyo washirika wa Kimataifa na wadau wa maendeleo wameombwa kuendelea kuwasaidia watetezi wa Haki za Binadamu na serikali kutafuta njia bora naya kudumu ya kutatua migogoro hiyo kwa maslahi ya pande zote mbili.
Social Plugin