KAMERA KUFUNGWA BUIGIRI KUKABILI AJALI BARABARA KUU DAR-DODOMA


Diwani wa Kata ya Buigiri Mhe Kenneth Yindi,akimueleza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka jinsi walivyojipanga kufunga Kamera ili kuzuia ajali zinazotokea kwa wanafunzi wakati wa kuvuka barabara katika eneo la Buigiri wakati wa uzinduzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Buigiri yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.


MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akimpongeza Diwani wa Kata ya Buigiri Mhe Kenneth Yindi,kwa wazo la kufunga Kamera ili kuzuia ajali zinazotokea kwa wanafunzi wakati wa kuvuka barabara katika eneo la Buigiri wakati wa uzinduzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Buigiri yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.


Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga,akizungumza wakati wa uzinduzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Buigiri yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.


MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akiwa amekaa ndani ya darasa mara baada ya kuzindua vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Buigiri yaliyojengwa kwa mradi wa Fedha za Kupambana na UVIKO-19 wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

................................................................

Na.Alex Sonna,Chamwino

KUTOKANA na idadi kubwa ya wanafunzi kugongwa na magari na kupoteza maisha katika Barabara kuu ya Dodoma - Dar es Salaam halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma anapanga kufunga kamera katika eneo la Buigiri kwa ajili ya kunasa magari yanayopita kwa mwendo kasi.

Hayo yameelezwa na Diwani wa Kata ya Buigiri Mhe. Kenneth Yindi,mbele ya Mkuu wa Mkoa Dodoma wakati akizindua vyumba vya madarasa yaliyojengwa kwa fedha za UVIKO-19, katika shule ya sekondari wa Buigiri.

Yindi, amesema kuwa kata hiyo ina shule sita na barabara kuu imepita katika vijiji vitatu.

"Wanafunzi wengi wanagongwa, magari yanakimbia sana hasa yale ya serikali, wanafunzi na hata wananchi wanapoteza maisha kutokana na ajali za barabarani" amesema Yindi

Aidha, amesema alitembelea maeneo mbalimbali nchini yaliyopitiwa na barabara kuu ili kuona namna gani wataweza kuepukana na ajali hizo.

"Tumeshafanya kikao na kamanda wa kikosi cha usalama barabarani na kupeleka ombi rasmi kwa kutumia wataalam wa ICT tutafunga kamera nne” alisema

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka, amesemasuala la kufungwa kamera ni jambo zuri kwani litasaidia kuokoa maisha wanafunzi katika shule hizo pamoja na watu wote wanao itumia barabra hiyo.

"Fungeni hizo kamera huenda tukapata suluhisho la ajali ambazo zimekuwa zikijitokea katika eneo hili mara kwa mara na kukatisha uhai wa vijana wetu" amesema.

Aidha alimtaka mkuu wa wilaya ya Chamwino Gift Msuya na vyombo vya ulinzi na usalama kuona jinsi gani jambo hilo linatekelezwa kwa haraka.

Awali akipokea taarifa ya ujenzi wa madarasa ilielezwa kuwa Buigiri Sekondari ilipokea jumla ya Sh. milioni 60 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa matatu na ofisi ya walimu.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbanga, amesema Chama hicho kinawashukuru wote waliohakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post