KIUNGO, Udoh Utop jana Jumapili aliondoka rasmi nchini ambapo alikuja kwa ajili ya majaribio ndani ya Simba na kurejea kwao nchini Nigeria.
Udoh alikuja nchini sambamba na winga mwenye uraia wa Ivory Coast, Cheick Mounkoro na Sharaf Shiboub waliofanya majaribio na Simba katika michuano ya Kombe la Mapinduzi lakini hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kupata mkataba.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Udoh Utop alisema kuwa tayari ameshaondoka kurejea kwao nchini Nigeria ambapo kuna ofa nyingine amezipata, lakini kama kuna timu itakuwa ipo tayari kumsajili kutoka Tanzania yupo tayari kujiunga nayo.
“Tayari safari yangu imeiva na leo (jana) Jumapili nitaondoka kuelekea Nigeria ambapo ni nyumbani, kuna ofa nimepata kutoka timu nyingine sehemu mbalimbali nakwenda kuziangalia baada ya kushindwa kusajiliwa na Simba.
“Kuhusu Tanzania nimependa mazingira yake na soka lake hivyo kama kutakuwa na timu yoyote kutoka Tanzania itanihitaji basi nipo tayari kujiunga nayo,” alisema kiungo huyo.
STORI: MARCO MZUMBE, Dar es Salaam
Social Plugin