MWANAMKE mmoja mwenye umri wa miaka 26 ambaye ni Mama wa Watoto wawili amejiua kwa kujinyonga baada ya kuwaua kwa sumu Watoto wake wawili wa kike (mmoja ana umri wa miaka miwili na mwingine mitano) katika Kijiji cha Katitika kilichopo Kaunti ya Muranga nchini Kenya.
Polisi nchini Kenya wamethibitisha na kusema uchunguzi unaendelea na kwamba Mama huyo ameacha ujumbe unaohisiwa umemlenga Mumewe, unaosomeka… “Asante Mpendwa wangu kwa ulichonifanyia na nakuaga bye bye bye, niliwatunza Wazazi wako lakini haukujali, Asante.”
“Endelea na maisha yako, tafuta mwingine wa kumleta nyumbani kwako lakini kumbuka hakuna atakayeishi kwa amani, nakutakia maisha mema…”
Social Plugin