Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika Stephen Masele amempongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kumuomba Radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Kupitia Ukurasa wake wa Twitter Stephen Masele andika ujumbe huu:
"Hongera mhe Spika kwa kumuomba radhi Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kuwaomba radhi watanzania. Huo ndio uungwana"
Hongera mhe Spika kwa kumuomba radhi Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kuwaomba radhi watanzania. Huo ndio uungwana. pic.twitter.com/cMslP7GFf5
— Stephen Julius masele (@stephen_masele) January 3, 2022
Mapema leo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amemuomba radhi Rais Samia Suluhu Hassan na Watanzania wote ambao waliupokea ujumbe wake kitofauti kuwa yeye ni miongoni mwa watu wanaopinga jitihada zinazofanywa na Rais katika kuliletea Taifa maendeleo.
Pia amewahakikishia watanzania yeye ni yule yule ni uimara wake upo palepale na wale waliomrushia matusi amewasamehe bure na wengine hawajui wayatendayo na ndio maana amebeba matusi yote hivyo amekosa na asamehewe.
“Kwa hiyo binafsi yangu popote pale ambapo nilihisiwa kwamba nimetoa neno la kumvunja moyo Rais wetu na akavunjika moyo, ninatumia fursa hii kupitia kwenu kumuomba radhi sana mheshimiwa Rais na kwa Watanzania wote,”amesema.
Social Plugin