Waziri wa Mambo ya Ndani Nchi Mhandisi Hamad Masauni akiongea na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara -Mtumba Jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni akiwa na watendaji wa ngazi za juu wa Jeshi la polisi nchini.Na Ditto Kwilasa,Malunde 1 Blog -DODOMA.
WIZARA ya mambo ya ndani ya nchi imeunda kamati ya kuishauri Serikali kuhusu namna ya kufanya katika kupata suluhisho la kudumu katika kuzui uhalifu na mauaji yaliyokithiri nchini huku ikitoa siku 21 kukamilisha kazi yake na kurudisha mrejesho kwenye wizara hiyo.
Hatua hii imekuja zikiwa zimebakia siku mbili tu mara baada ya Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Isdory Mpango kutoa siku saba kwa Jeshi la polisi nchini na idara zake zote kutafuta ufumbuzi wa mauaji yanayoendelea nchini
Hayo yameelezwa leo Januari 31,2022 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni wakati akiongea na waandishi wa habari Jijini Dodoma mara baada ya kikao chake na uongozi wa ngazi ya juu wa Jeshi la polisi ili kutoa mrejesho wa matokeo ya kilichojadiliwa kuhusu kadhia ya matukio ya mauaji yanayoendelea nchini.
Amesema kuundwa kwa kamati hiyo kutasaidia kupatikana kwa suluhisho la kudumu katika kuzuia mauaji na uhalifu mwingine nchini huku akitaka watanzania kutoa ushirikiano katika kuwabaini wahalifu.
Masauni amesema,kamati hiyo itahusisha jopo la wataalam kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo Wizara ya mambo ya ndani ya nchi,Tamisemi,Jeshi la polisi,Ofisi ya wakili mkuu wa Serikali,Ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali,Usalama wa Taifa,Ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka,Takukuru,Wizara ya habari na elimu ya juu.
Sambamba na hayo ameeleza kuwa kutokana na kukithiri vitendo vya mauaji nchini hadi sasa Jeshi la polisi linawashikilia watu zaidi ya 150 huku akitaja mikoa vinara kwa mauaji kuwa ni Kagera, Dodoma,Mara ,Songwe na Kigoma.
Ametaja sababu mbalimbali za mauaji hayo kuwa ni pamoja na imani za kishirikina,wivu wa mapenzi,wivu wa maendeleo,visasi,migogoro ya ardhi,mali na ulevi na kueleza kuwa Serikali haiwezi kukaa kimya na kudharau malalamiko ya wananchi .
Social Plugin