Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MJAMZITO AUAWA BAADA YA KUGOMA KWENDA KWA MGANGA WA KIENYEJI


Jeshi la Polisi mkoani Songwe linamshikilia mkazi wa Kata ya Mlale wilayani Ileje, Shukrani Kamwela mwenye umri wa miaka 16 kwa tuhuma za mauaji ya mwanamke mjamzito, Subira Kibona ambaye alikuwa na umri wa miaka 16.

Kamanda wa polisi mkoani humo, Janeth Magomi amesema kuwa mtuhumiwa huyo anadaiwa kumuua Subira ambaye walikuwa wanaishi pamoja kama ‘mke na mume’ kwa kumchoma na kitu chanye ncha kali kwa kile kilichoelezwa kwamba ni marehemu kukataa kupelekwa kwa mganga wa kienyeji.


Taarifa zaidi zinaeleza kwamba Subira alitoweka tangu Januari 13 ambapo wananchi walifanya jitihada za kumtafuta ambapo baadaye, Januari 16, 2022 mwili huo ulikutwa ukiwa na jeraha la kuchomwa na kitu chenye ncha kali huku ukiwa umeteketezwa kwa moto na kutupwa katika korongo porini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com