Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MRADI WA AKILI BANDIA WAZINDULIWA UDOM



Serikali ya Tanzania imezindua mradi wa maabara ya akili bandia (artificial intelligence) utakaosaidia kurahisisha shughuli za maendeleo nchini.

Hayo yamesemwa jana Jumatatu Januari 24, 2022 na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohamed Khamis Abdullah akizindua mradi huo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

“Kama hivi wengi tunavyoangalia dunia za sasa hivi wenzetu wameshakwenda mbele zaidi. Sometimes (wakati fulani) unakuta watu wanavyokwenda makazini wanajibiwa na robot, unapopanda lifti, mwendo kazi,” amesema.

Naibu Waziri huyo amesema teknolojia hiyo inatumika hata mashambani ambapo badala ya kwenda mtu linatumika robot na maofisini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com