Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, amesema uchunguzi umebaini kuwa mshumaa uliowashwa na mateja ndio sababu ya kuungua kwa soko la Karume na kusema anaamini jeshi la polisi litakuchua hatua stahiki kwa wahusika kwa kuwa wanajulikana.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 24, 2022, mara baada ya kupokea taarifa ya tume iliyoundwa ili kuchunguza ni nini hasa chanzo cha moto huo uliotokea usiku wa kuamkia Januari 16 mwaka huu na kupelekea karibu asilimia 98 ya soko la Karume kuteketea kwa moto.
“Sasa zile hisia za nani kachoma nini, mmeona wenyewe, tumeelezwa na mmemsikia Jose amejitoa mhanga ameeleza kwamba tusipoteze muda aliyechoma soko ninamjua, ninaamini jeshi la polisi litachukua hatua stahiki kwa sababu watu hao wanajulikana,” amesema RC Makalla.
Miongoni mwa maoni na Mapendekezo ya Kamati ni pamoja ujenzi wa soko jipya linaloendana na hali ya sasa na vizimba kutolewa kwa kipaumbele kwa Wazawa, uwepo wa mfumo mzuri wa kuzuia moto, Barabara za kuingia na kutoka, ujenzi wa majengo ya muda mfupi, kila mfanyabiashara kuwa na Bima.
Social Plugin