RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo Januari 8,2022 amefanya uteuzi wa baadhi ya makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu na kuwahamisha baadhi na wengine kubakishwa vituo vyao vya kazi kama ifuatavyo;
Makatibu wakuu
Rais Samia amemteua Dkt.Francis K.Michael, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utali.
Pili, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Adolf H.Ndunguru, Naibu Katibu Mkuu (Sera), Wizara ya Fedha kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Madini;
Tatu, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Prof.Jamal A.Katundu, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu).
Nne, Mheshimiwa Rais Samia amemteua, Dkt.Jim J.Yonazi, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Tano, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Balozi Mhandisi Aisha S. Amour aliyekuwa Balozi Kuwait kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi).
Sita, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Profesa Eliamani M. Sedoyeka, Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Saba, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Mhandisi Felshesmi J.Mramba, Kamishina wa Nishati kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati.
Social Plugin