Panya shujaa wa Tanzania aliyetumika kutegua mabomu yaliyotegwa ardhini na vilipuzi -Magawa amefariki dunia mwishoni mwa wiki.
Mwezi November mwaka jana Magawa alitimiza umri wa miaka minane na alistaafu pia mwaka jana kutokana na uzee wake kwakuwa alianza kupunguza kasi ya kutegua mabomu.
Magawa alizaliwa Morogoro, Tanzania November 5,2014 akiwa na uzani wa KG 1.2 na urefu wa Sentimita 70 na hadi anakufa amenusa mabomu na silaha nyingine zaidi ya 100.
Kupitia taarifa katika ukurasa wake wa Instagram. Shirika la HeroRat limesema Magawa alikuwa na afya njema wiki jana lakini afya yake ilianza kudhoofika mwishoni mwa wiki na kuaga dunia akiwa na umri wa miaka minane.
Magawa alifunzwa na shirika la uhisani la Apopo nchini Ubelgiji lenye makao yake nchini Tanzania, ambalo limekuwa likiwalea wanyama hao wanojulikana kama HeroRATS{Panya shujaa} kubaini mabomu ya ardhini tangu 1990.
Social Plugin